Makala namba (1) .
قال المزني – رحمه الله-:
Amesema Al-muzaniy- Allah amrahamu-:
دخلتُ على الشافعي، رضي الله عنه، عند وفاته
Niliingia kwa Shafii -Allah amridhie- wakati wa kifo chake
فقلت له: كيف أصبحت يا أستاذ؟
Nikamwambia:(Hali yako) ipoje ewe ustadhi ?
فقال: أصبحت من الدنيا راحلا، ولإخواني مفارقا،
Akajibu: Nimekuwa ni mwenye kuondoka duniani, na ni mwenye kuachana na ndugu zangu,
وبكأس المنية شاربا، وعلى الله واردا، ولسوء أعمالي ملاقيا،
na (nimekuwa) ni mwenye kunywa glasi ya kifo , na ni mwenye kuwasili kwa Allah, na ni mwenye kukutana na matendo yangu mabaya,
فلا أدري نفسي إلى الجنة تصير فأهنيها، أو إلى النار فأعزيها
basi wala sijui nafsi yangu itaingia peponi niipongeze au itaingia motoni niipe pole .
تاريخ دمشق لابن عساكر ،ج ٥٣ ص ٤٣١ من الشاملة .
Maelezo ya mwandishi:
Hapo imamu shafii -Allah amrahamu- aliposema kuwa : Yeye ni mwenye kukutana na matendo yake mabaya , na pia pale aliposema kuwa hajui kuwa nafsi yake itaingia peponi aipongeze au motoni aipe pole.
Hii ni alama ya watu wenye kufanya matendo yao mema kwa ajili ya Allah siku zote huzituhumu nafsi zao kuwa hazijatekeleza haki za Allah kama alivyosema Allah -aliyetukuka- :
وَٱلَّذِينَ يُؤْتُونَ مَآ ءَاتَواْ وَّقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَىٰ رَبِّهِمْ رَٰجِعُونَ
“Na wale ambao hutoa waliyopewa,na hali nyoyo zao zinaogopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi “
المؤمنون ٦٠
Ufafanuzi:
Hii ni katika alama ya watu wema nayo ni kutoa vile wanavyovitoa kama zaka ,sadaqa ,na hufanya matendo mbalimbali na hali nyoyo zao zina hofu kuwa hayo matendo yao hayajakubaliwa kwa mapungufu waliyokuwa nayo ,na wanaona kuwa hayo matendo yao hayatowaokoa na adhabu.
Mama Aisha- Allah amridhiel- alimuuliza Mtume- swala na salamu za Allah zumfikie – maana ya aya hii akasema:
أَهُمُ الَّذينَ يشربونَ الخمرَ ويسرِقونَ؟
Je hao ni wale ambao wanakunywa pombe na wanaiba ?
قالَ : لا يا بنتَ الصِّدِّيقِ ، ولَكِنَّهمُ الَّذينَ يصومونَ ويصلُّونَ ويتصدَّقونَ ،
(Mtume) akasema: Hapana ewe binti Swiddiq lakini hao ni wale ambao wanafunga na wanaswali na wanatoa sadaqa,
وَهُم يخافونَ أن لا تُقبَلَ منهُم
na hali wanahofu ya kutokubaliwa (hizo ibada)
” أُولَئِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ“
“ Basi hao ndio wanaokimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao tangulia kuyafikia ”
صحيح الترمذي.
Inaendelea ..Allah akitaka .
Mwandishi : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 30, 1443H ≈ Jan 3, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•