كتب الشيخ صالح العصيمي -حفظه الله تعالى- عبر حسابه على تويتر .
Ameandika sheikh Swaleh Al-Uswaim -Allah amuhifadhi- kupitia ukurasa wake wa twitter (maneno yafuatayo) :
ربح من صان لسانه عن مشاتمة الطاعن،ودفع أذاه برفق ولين،
Faida ya aliyeuhifadhi ulimi wake kwa kutomtukana mwenye kumtukana, na akayaondoa maudhi yake kwa upole na ulaini
قال السعدي :
Amesema Assadiy :
«من آذاه الناس بالأقوال البشعة،فصان لسانه عن مشاتمتهم،ودفع عن نفسه برفق ولين؛
Yule ambaye watu wamemuudhi kwa maneno mabaya, na akaulinda ulimi wake kwa kujiepusha na kuwatukana, na akaitetea nafsi yake kwa upole na ulaini
اندفع عنه مِن أذاهم بسبب ذلك مالا يندفع عمَّن قابلهم،وصنع كصنيعهم،
(basi) kutaondoka kwake katika maudhi yao kwa sababu ya (tabia) hiyo, yale ambayo hayaepukani kwa yule aliyekabiliana nao (kwa maneno) na akafanya kama walivyofanya,
مع راحته وطمأنينة قلبه،واكتسابه للرزانة والحلم،وتنزهه عن سفسفة الأقوال».
pamoja na raha ya (nafsi) yake na utulivu wa moyo wake,na (faida nyingine ni kule) kuchuma kwake (tabia ya) utulivu na upole na kujitenga kwake mbali na maneno yasiyokuwa na maana
السبت ٢١ المحرم ١٤٣٦ه
Maelezo ya mfasiri:
Hizi ni miongoni mwa faida za kuuhifadhi ulimi kwa kutomrudishia yule aliyekutukana, na kufanya kwako hivi utakuwa umeiondolea maudhi nafsi yako na pia ni sababu ya kupata raha na utulivu wa moyo na pia utakuwa umejifunza tabia ya upole na utulivu.
Lakini kuna baadhi ya watu hawawezi kunyamaza bali wakiguswa tu wanasema!tena huwenda wakazungumza mpaka wakachupa mipaka kwa kumdhulumu yule anayemjibu,na baya zaidi huwenda baadhi ya watu wakamsema mtu aliyefariki na kumbananga bila ya haja ya kisheria kwa kisingizio cha kujeruhi na kuadilisha ! na bila shaka tendo hili ni uovu na kosa na hata tuseme kuwa amekosea, hayo makosa nayo hupimwa katika mizani ya kisheria na tukumbuke kuwa Mtume wetu -swala na salamu za Allah zimfikie – amesema -:
”- لا تَسُبُّوا الأمْوَاتَ، فإنَّهُمْ قدْ أفْضَوْا إلى ما قَدَّمُوا “
“ Msiwatukane maiti kwa sababu wao bila shaka wameyafikia yale waliyoyatanguliza (duniani)”
رواه البخاري
Uchambuzi wa hadithi:
Ndugu yangu kumbuka kuwa unapomtukana maiti au kumsema vibaya yeye hayampati hayo unayoyazungumza kwa sababu yeye kwa sasa amekutana na malipo ya yale aliyoyatenda hapa ulimwenguni, isipokuwa kinachotokea unapomtukana au ukamsema vibaya huyo maiti ni sababu ya kuleta huzuni kwa waliokuwa hai na kusababisha mivutano na magomvi kwa sababu unapomtukana au ukamsema vibaya kumbuka kuwa huyu ana ndugu na marafiki na wao pia huwenda watazungumza na kujibu na matokea yake ni kutupiana maneno , na ndiyo maana Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- akasema:
” لا تسبُّوا الأمواتَ فتُؤذوا الأحياءَ“
Msiwatukane maiti mkawaudhi waliokuwa hai .
رواه الترمذي
Haifai kumtukana maiti au kutaja mabaya yake kwa mtu ambaye tunafahamu kuwa ni mtu mwema ,ama yule ambaye tunajua uovu wake kama vile makafiri mbalimbali ambao walikuwa ni maadui wa uislamu kama vile Abuu Jahl na wengineo na pia wanafiki au mtu ambaye anajulikana kuwa alikuwa maovu kwa kudhihirisha bidaa yake ambayo alikuwa akiwalingania watu katika bidaa hiyo au aliandika vitabu vyenye upotevu au kukawepo watu walioshikamana na bidaa hiyo basi muda huo itaruhusiwa kutajwa makosa ya maiti huyu ili watu wamtahadhari hata kama ni muislamu .
Tanbih:
Kusema kuwa mtu fulani ameingia katika bidaa kunatakiwa vigezo vya kisheria vitimie, na wala si suala la kufuata mkumbo tu na haswa katika zama hizi ambazo fitna zimekithiri na kumuingiza mtu katika bidaa ni suala jepesi mno kupita kiasi na kuna watu wamefungua vinywa vyao kama kasuku katika hili !
Tunamuomba Allah atufishe katika uislamu na sunnah .
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 29, 1445H ≈ Aug/4, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•