FAIDA YA KUTOFUATILIA MAKOSA YA WATU!

‏قَالَ الْعَلَّامَةُ السِّعْدِيُّ ـ رَحِمَهُ اللهُ ـ :
Amesema mwanawachuoni mkubwa Assi’idiy-Allah amrahamu-:

«مَنْ تَغَافَلَ عَنْ عُيُوبِ النَّاسِ وَ أَمْسَكَ لِسَانَهُ عَنْ تَتَبُّعِ أَحْوَالِهِمْ الَّتِيٰ لَا يُحِبُّونَ إِظْهَارَهَا : 

Mwenye kutoangalia kasoro za watu, na akauzuia ulimi wake kufuatilia hali zao ambazo hawapendi zidhihirike :

سَلِمَ دِينُهُ وَ عِرْضُهُ،
وَ أَلْقَىٰ اللهُ مَحَبَّتَهُ فِيٰ قُلُوبِ الْعِبَادِ،‏ وَ سَتَرَ اللهُ عَوْرَتَهُ،

(mtu huyo) itasalimika dini yake (mbele ya Allah) na heshima yake (mbele za watu), na Allah atatia mapenzi yake katika nyoyo za waja na atazistiri kasoro zake,

فَإِنَّ الْجَزَاءَ مِنْ جِنْسِ الْعَمَل، وَ مَا رَبُّكَ بِظَلَّامٍ لِلْعَبِيد».

kwani hakika malipo ni jinsi ya matendo

“Na Mola wako Mlezi si mwenye kumdhulumu mja”

الْفَوَاكِهُ الشَّهِيَّةُ ١١٢/١

Maelezo ya mfasiri:

Miongoni mwa sifa za muislamu ni kutofuatilia kasoro za watu na kuuzuia ulimi wake kufuatilia hali mbalimbali za watu ambazo wenyewe hawapendi zijulikane kwa wengine, na yule aliyeshikamana na tabia hii njema atapata faida nyingi hapa hapa duniani kwanza kabla ya ahera na miongoni mwa hizo ni hizi alizozitaja sheikh hapa nazo ni :

1- Dini yake itasalimika kwa Allah kwa maana atakuwa ni mtu mwenye dini iliyotimia na mwenye imani iliyokamilika,
na heshima yake itahifadhika kwa watu ina maana watu hawatomsema vibaya na wala hawatomfuatilia na kumpeleleza.

2-Allah atatia katika nyoyo za watu mapenzi kwake kwa maana watu watakuwa wanampenda .

3- Allah atazistiri kasoro na makosa yake .

Na bila shaka uislamu umeiharamisha tabia hii ya kuwapeleleza watu na kuwafuatilia kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

يا معشرَ من آمنَ بلسانِه ولم يدخلْ الإيمانُ قلبَه ،

“Enyi kundi la wale walioamini kwa ndimi zao na haikuingia imani katika nyoyo zao ,

لا تغتابوا المسلمين ، ولا تتَّبعوا عوراتِهم ،

Msiwasengenye waislamu na wala msifuatilie makosa yao,

فإنه من اتَّبعَ عوراتِهم يتَّبعُ اللهُ عورتَه ، ومن يتَّبعِ اللهُ عورتَه يفضحُه في بيتِه.

basi hakika hali ilivyo yule mwenye kufuatilia makosa yao (waislamu) Allah atayafuatilia makosa yake na yule ambaye Allah atayafuatilia makosa yake atamfedhehesha (hata akiwa ndani ya nyumba yake) .

رواه أبو داود.

Ufafanuzi wa hadithi :

Katika hadithi hii Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- anatoa tahadhari kutokana na dhambi ya kusengenya na msengenyi imani yake haijakamilika, na akatahadharisha dhambi ya kufuatilia makosa ya watu na kuwapekua na akasema kuwa mwenye kufuatilia makosa ya waislamu basi Allah atamletea mtu atakayekuja kumfedhehesha hata akiwa ndani ya nyumba yake amejificha na watu hawamuoni basi hiyo fedheha itampata .

Tanbih:

Sheikh -Allah amrahamu- amesema kuwa mwenye kuyastiri makosa ya waislamu basi Allah atayastiri makosa yake kama alivyosema Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-:

” من ستر مسلما ستره الله في الدنيا والآخرة “

“ Mwenye kumstiri muislamu Allah atamstiri duniani na akhera ”

رواه ابن ماجه .

Makusudio ya muislamu anayestiriwa ni ambaye hajulikani kwa maovu na wala si mashuhuri kwa hayo, mtu kama huyu ikitokea ameteleza kwa kufanya kosa basi ni wajibu astiriwe,ama yule aliyekuwa maarufu kwa maovu na amezama ndani yake na mwenye kuyaendea mbio hayo maovu mtu huyu akionwa anafanya maovu hastahiki kustiriwi bali jambo lake lifikishwe kwa mtawala ili amzuie kufanya uovu huo .

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 21, 1445H =Apr 30, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *