FATWA MUHIMU KWA WENYE VIPANDWA .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

FATWA MUHIMU KWA WENYE VIPANDWA

السؤال (٥٠٣)
Swali (503)

سئل العلامة الفوزان- حفظه الله-

Aliulizwa mwanachuoni mkubwa Al-fauzan- Allah amuhifadhi-

أحيانًا وأنا أقود سيارتي بسرعة تتعرض لي بعض القطط أو الكلاب؛ فلا أستطيع السيطرة على السيارة، فأدهسها على الرغم مني؛ فهل عليَّ إثم في هذا أم لا‏؟‏

Kuna baadhi ya nyakati nakuwa naendeesha gari kwa haraka hutokea (mbele yangu) baadhi ya paka au mbwa na (nakuwa) siwezi kuimiliki gari ,(kinachotokea huwa) nawagonga bila ya kupenda ,je napata madhambi katika hili au ?

الجواب
Jawabu :

الحيوانات لها حرمة، لا يجوز الاعتداء عليها وقتلها؛ إلا إذا كانت مؤذية؛ كالسباع والحيات والأشياء المؤذية، أما الحيوانات غير المؤذية؛ فهذه لا يجوز قتلها،

Wanyama wana utukufu ,haifai kuwafanyia uadui na kuwaua ,isipokuwa wakiwa ni wenye kuudhi kama wanyama wakali ,na nyoka na vitu vyenye kuudhi ama wanyama wasioudhi hawa haifai kuwaua,

وإذا كانت عرضت لك في طريق وأنت في السيارة؛ فعليك أن تحافظ على حياتها، وأن تترك لها فرصة المرور،
na wakiwa hao ( wanyama) wamekutokea njiani na hali wewe upo ndani ya gari ,basi unawajibika kuhifadhi uhao wao na uwaachie njia ya kupita ,

أما إذا لم تتمكن من ذلك، ودهستها من غير قصد، ولم تتمكن من الامتناع عنها؛

ama muda ambao haukuwa na uwezo wa hilo na ukawakanyaga (ukawagonga) bila ya kukusudia ,na (wanyama) hawakuweza kujizuia kutokana na hilo (gari) ,

فلا حرج عليك من ذلك، إنما تأثم لو تعمدت قتلها بدون مبرر؛ لأنها حيوانات لها حرمة وليست مؤذية .

basi hakuna ubaya juu yako kwa hilo ,hakika si vinginevyo utapata madhambi lau utakusudia kuwaua bila ya sababu ,kwa sababu hao ni wanyama (na) wana utukufu / heshimika na hawamuudhi (mtu).

المنتقى من فتاوى الشيخ الفوزان

Maelezo ya mfasiri:

Haifai kuwatesa wanyama na kila kiumbe chenye roho ila wale ambao wamevuliwa na sheria kwa kuruhusiwa kuwaua kama wale wenye kuudhi na kudhuru ,hebu soma hadith hii utaona namna uislamu ulivyoamrisha kuwafanyia huruma wanyama na utaona huruma wa mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- :

عن عبد الله بن مسعود – رضي الله عنه-قال:

Kutoka kwa Abdullah bin Masu’ud (Allah amridhie) amesema:​

كنا مع رسول الله في سفر, فانطلق لحاجته, فرأينا حمرة معها فرخان, فأخذنا فرخيها,
فجاءت الحمرة, فجعلت تفرش- ترفرف – فجاء النبي-صلى الله عليه وسلم-فقال:{{من فجع هذه بولدها؟ ردوا ولدها إليها}}

“{{Tulikuwa safarini pamoja na mjumbe wa Allah,akatoka kwa ajili ya kujisaidia (ghafla) tukamuona ndege akiwa na makinda mawili tukayachukua (makinda) yake,(mara) akaja (yule) ndege. (mama wa makinda) akaanza kurukaruka (na kuzunguka) ,mara akaja Mtume (swala na salamu za Allah zimfike) na akasema:

“Ni nani aliyemhofisha huyu (ndege) kwa kumchukulia wanawe? mrudishieni wanawe”

​{رواه أبو داود }​

[ Ameipokea Abuu Dawuud ]

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 26, 1442H ≈ Jun 7, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *