FUNGA YA ‘ASHURAA KUNAPOTOKEA MKANGANYIKO KATIKA MWEZI MUANDAMO.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

NAMNA YA KUFUNGA FUNGA YA ‘AASHURAA /TAREHE 10 MFUNGO NNE PINDI KUTAPOTOKEA MKANGANYIKO WA MUANDAMO WA MWEZI .

روي عن النبي – صلى الله عليه وسلم – أنه قال:

Imepokewa kutoka kwa Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake – kwamba amesema:

{خالفوا اليهود و صوموا يوما قبله ويوما بعده}

{ Nendeni kinyume na Mayahudi na fungeni siku moja kabla yake (‘Aashuraa) na siku moja baada yake }

Takhriji ya hadithi hii kuhusiana na funga ya ‘Aashuraa ambayo ameitaja Sheikh Ibn Baaz – Allah amrahamu – katika fatwa yake ni hii hapa chini:

ذكره العيني في عمدة القارئ في الصوم باب صيام يوم عاشوراء ج 11 ص 116 وذكره صاحب الفتح الكبير في حرف الصاد باب صوم يوم عاشوراء برقم 7293.

​Hii ni takhriji fupi ya hadithi hii ambayo wanachuoni wametofautiana juu ya usahihi wake, kuna wale walioidhoofisha kama Sheikh Al-baaniy na wengineo kutokana na mmoja ya wapokeaji wake ambaye ni ibnu abii Lailaa ambaye hifdhi yake ni mbaya,

Lakini udhaifu kama huu haudhuru katika hadithi kuitumia katika masuala ya fadhila za ibada ndiyo maana baadhi ya wanachuoni wakasema kuwa katika miongoni mwa daraja za funga ya ‘Aashuraa ni kufunga siku tatu yaani: Siku ya tisa na siku ya kumi ambayo ni ‘Aashuraa yenyewe na siku ya kumi na moja,

​Na msimamo wa kufunga siku tatu ni wa baadhi ya wanachuoni kama Asshaukaaniy na wengine wamesema kwamba inatakiwa mtu afunge siku tatu kama kukitokea mkanganyiko mwanzoni mwa mwezi muandamo yaani kukawa hakuna uhakika wa usahihi wa tarehe kama vile mwaka huu, kwa hiyo atafunga siku tatu ili kuchukua tahadhari na atakuwa ameipata siku ya ‘Aashuraa kama alivyonukuu Ibnu Qudaamah kutoka kwa Imamu Ahmad katika Al-mughniiy,

Na wengine wanaona kuwa mwenye kufunga siku tatu atakuwa amepata fadhila za kufunga siku tatu za kila mwezi kama kama alivyoeleza sheikh ibnu ‘Uthaimin, pamoja na kuwa kuna wanaolipinga hili lakini kusitokee mzozo baina yetu kuhusu hili ama kauli ya kusema kuwa kufunga siku tatu ni bida’a!! hii hatuikubali,

​Ukaraha wa kufunga siku ya kumi peke yake ya mwezi wa Muharram ni kauli ya baadhi ya wanachuoni na si wote waliosema hivyo wengine wanaona kwamba hakuna ukaraha wa hilo kama vile Al-imaamu ibnu Taimiyyah. Lakini ni vizuri kuongeza siku ya tisa au ya kumi na moja.​

📚 ​كتب أبو ثرياء إسماعيل بن سيف امبوندي​ الشافعي

Ameyaandika Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Assha’afiy .

​حامدا مصليا، بعد عصر الأربعاء السابع من شهر الله المحرم سنة ١٤٣٩ھ​.

Hali ya kumsifu (Allah) na kumswalia (mtume), Baada ya Al-asiri, Jumatano (tarehe) 7 mwezi wa Allah wa Muharram/Mfungo nne mwaka 1439H.

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Toleo la pili: Mfungo nne 5, 1443H ≈ August 13, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *