Furaha ya kweli !

◾️قال ابن القيم – رحمهُ الله- :

Amesema ibn l-Qayyim -Allah amrahamu -:

•السعادة الحقيقية، وهي سعادةٌ نفسائيةٌ روحية ٌ قلبية،

Furaha ya kweli hiyo ni furaha ya kinafsi ya kiroho ya kimoyo

وهي سعادة العلم النافع و ثمرتُهُ فإنها هي الباقية على تقلُّب الأحوال ،

Nayo ni furaha ya elimu yenye manufaa na matunda yake bila shaka ni yenye kubakia katika hali zote,

والمصاحبةُ للعبد في جميع أسفاره وفي دوره الثلاثة

Na (ni furaha) yenye kuongozana na mja katika safari zake zote na katika nyumba zake tatu

أعني دار الدنيا ودار البرزخ، ودار القرار وبها يترقَّى في معارج الفضل و درجات الكمال.

Nakusudia nyumba ya dunia, na nyumba ya kizuizini (kaburini), na nyumba ya daima, na katika (nyumba) hiyo (ya ahera) atapanda ngazi za (daraja) la ubora na daraja za ukamilifu

📚 مفتاحُ دارِ السعادة 1 / 297-298 ].

Maelezo ya mfasiri:

Furaha ya elimu ya kisheria ni yenye kuambatana na mja sehemu zote : Duniani ,kaburini na ahera .

Duniani furaha na raha ya elimu hailingani na furaha yoyote na wanawavyuoni huhisi furaha ya hali ya juu pindi wanaposoma vitabu kama anavyosema ibn Jauziy -Allah amrahamu -:

”وإني لأخبر عن حالي ما أشبع من مطالعة الكتب، وإذا رأيت كتاباً لم أره، فكأني وقعت على كنز“

“Na hakika mimi naielezea hali yangu : (mimi) sishibi kusoma vitabu na pindi nikionapo kitabu nisichokiona (kabla ya hapo), basi (nakuwa) kanakwamba nimepata hazina ”

صيد الخاطر (٣٥٨)

Kuna tukio la ajabu na la kufurahisha linalojulisha mapenzi na raha wanayoipata wanawachuoni pindi wanaposoma vitabu mpaka inafikia mmoja wao hahisi hata hatari iliyomfikia!

Huyu hapa mwanachuoni mkubwa wa hadithi na fiqih Abdul-Haqq bin Seiph Ddin Addahlaw -Allah amrahamu:

كان دائم الاشتغال، مكبًّا على المطالعة في دياجير الليالي،

Alikuwa daima ni mwenye kushughulika (na) mwenye kuviinamia vitabu kwa kuvisoma katika giza la usiku,

حتى إنه قد احترَقَت عمامته غير مرَّة بالسراج الذي كان يجلس أمامه للمطالعة،

Mpaka kilemba chake kiliungua zaidi ya mara moja kwa (moto) wa taa ambayo alikuwa (akiiweka) mbele yake kwa ajili ya kusoma

فما كان يتنبه له حتى تتَّصل النار ببعض شعره.

basi alikuwa hazinduki kwa hilo mpaka moto unashika nywele zake .

المصدر: الإعلام بمن في تاريخ الهند من الأعلام المسمى بـ (نزهة الخواطر وبهجة المسامع والنواظر) (5/ 553 رقم 320)

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tatu 15, 1445H ≈ Jun /21, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *