HAKUZAA LAKINI AMEACHA KUNDI KUBWA LA WATU WEMA LENYE KUMUOMBEA DUA!

قال عماد الدين أبو الفداء إسماعيل بن عمر بن كثير الشافعي – رحمه الله – :

Amesema ‘imadu ddin Abul-fidaa Ismail bin Umar bin Kathir Asshafiy- Allah amrahamu-:

” مات ابن تيمية ، فكشفت عن وجهه وقبلته ، وقد علاه الشيب أكثر مما فارقناه ،

Alifariki ibn Taimiyyah basi (nilipoingia ndani) niliufungua uso wake na nikaubusu , na bila shaka (nilimkuta) akiwa na mvi nyingi zaidi kuliko vile tulivyomuacha,

لم يترك ولداً صالحاً يدعو له ، لكنه ترك أمةً صالحةً تدعو له “

(na yeye ibn Taimiyyah) hakuacha mtoto mwema anayemuombea dua ,lakini yeye ameacha kundi kubwa la watu wema linalomuombea dua .

📚 البداية والنهاية 18 / 296

Maelezo ya mfasiri:

Kama ilivyothibiti kutoka kwa mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- kuwa mwanadamu anapofariki thawabu zake zote hukatika kwake isipokuwa vitu vitatu pekee thawabu zake hazikatiki na akataja katika hivyo vitatu :

أَوْ وَلَدٍ صَالِحٍ يَدْعُو له.

“au mtoto mwema anayemuombea dua”.

Lakini kuna baadhi ya watu wao hawakuacha watoto wema ila wameacha kundi kubwa la watu linalowaombea dua yenye kuendelea mpaka kiama, na katika hao ni huyu mwanawachuoni mkubwa ibn Taimiyyah Al-hambaliy -Allah amrahamu- yeye katika maisha yake hakuwahi kuoa kwa sababu ya kushughulika kwake na elimu na kwa sababu ya hali mbalimbali zilizomtokea katika maisha yake..

Lakini kazi aliyoifanya mwanawachuoni huyu ni kubwa mno ambayo ukiielezea katika zama zetu huwenda baadhi ya watu wakasema si kweli! ,na miongoni mwa hizo kazi alizoziacha ni vitabu alivyoviandika ambavyo vitaendelea kusomwa milele na milele mpaka pale ambapo Allah atataka, na kama walivyokuwa wakisema zamani :

الْكِتَابُ وَلَدُكَ الْمُخَلَّدُ

“Kitabu ni mtoto wako anayeishi milele” .

Katika mifano yake ni huyu ibn Taimiyyah-Allah amrahamu- ambaye amefariki miaka mingi iliyopita lakini mpaka leo hii anatajwa na kuombewa dua kila sekunde na kundi kubwa la watu wema kama alivyosema ibn Kathir-Allah amrahamu-, bila shaka amesema kweli mshairi pale aliposema:

فـفـز بعلم تعش حيـا ً به أبــدا

Faulu kwa (kuwa na) elimu utaishi hai milele kwa sababu ya hiyo (elimu)

الناس موتى وأهل العلم أحياء

Watu wote ni maiti na wanawachuoni wapo hai.

Allah amrehemu ibn Taimiyyah na awarehemu wanawachuoni wetu wote, nasisi tunamuomba Allah atupe elimu yenye manufaa kama walivyopewa wanachuoni wetu hawa.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 28, 1445H ≈ Ja 10, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

       •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *