HALI YA MWENYE KUIPENDA DUNIA

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://ww w.fawaidusalafiya.net

HALI YA MWENYE KUIPENDA DUNIA .

‏🕯 قال ابن القيم رحمه الله:

◾️ ومُحب الدنيا لا ينفك من ثلاث :
💥 همّ لازم
💥وتعب دائم
💥وحسرة لا تنقضي

Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:

Mwenye kuipenda dunia haepukani na (vitu) vitatu :

1- Dukuduku lenye kuendelea .

2- Tabu ya daima

3- Kuvunjika moyo kusikoisha .

⬅️ وذلك أن محبها لا ينال منها شيئاً إلا طمحت نفسه إلى ما فوقه.

Na hilo ni kwa kuwa mwenye kuipenda hiyo (dunia) hatopata chochote kutoka (katika hiyo dunia) isipokuwa nafsi yake hupenda cha juu yake .

📚 [ إغاثة اللهفان ١ / ٥٨

Maelezo:

Hii ndiyo hali ya mpenzi wa dunia siku zote huwa na dukuduku yaani machungu mengi katika nafsi yake na wasi wasi je atakipata kile anachokitaka katika dunia au laa ?.

Siku zote hupata shida na kuangaika katika kuitafuta dunia .

Siku zote hufunjika moyo na hupatwa na huzuni kubwa pindi anapokosa vitu mbalimbali vya kidunia .

Bila shaka kuifanya dunia ni kitu muhimu zaidi hupelekea hali hii ,ndio maana katika dua alizokuwa akiomba Mtume- swala na salamu. za Allah zimfikie – ni :

(..وَلاَ تَجْعَلِ الدُّنْيَا أَكْبَرَ هَمِّنَا ، وَلاَ مَبْلَغَ عِلْمِنَا ، ..)

..Na wala usiifanye dunia kuwa ndiyo makusudio yetu makubwa zaidi, na wala (usiifanye kuwa) ndiyo ukomo wa elimu yetu ..

Maana ya dua hii ni kuwa:

Tunamuomba Allah – asiifanye dunia kuwa ndiyo makusudio yetu kama vile kutafuta mali ,vyeo,n.k ,pamoja na kuwa tusisahau fungu letu ktk dunia lakini tusiitangulize .Na vile vile tunamuomba Allah asiifanye elimu ya dunia au kufikiri kwa ajili ya dunia ndiyo upeo wa fikira zetu bali aijalie elimu ya kumfahamu Allah ndiyo uwe ukomo wa elimu yatu

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 30, 1442H ≈ Jun 11, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *