HALI YA WAISLAMU WAOVU SIKU YA KIAMA .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

◾️السؤال:

Swali:

أحسن الله إليكم فضيلة الشيخ، ما الدليل من الكتاب والسنة على دخول الرجل المسلم العاصي النار، ومن ثم خروجه إلى الجنة ؟

Allah akufanyieni ihsani (ewe) sheikh mbora : Ni ipi dalili kutoka katika qurani na sunnah juu ya kuingia motoni muislamu muovu kisha kutoka na kuingia peponi ?

◾️جواب العلامة ابن عثيمين رحمه الله:

Jawabu la mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin-Allah amrahamu-:

▫️الدليل على هذا حديث عن النبي عليه الصلاة والسلام ورد كثيراً في أن عصاة المؤمنين يدخلون النار يعذبون فيها بقدر ذنوبهم ثم يخرجون منها،

Dalili juu ya hili ni hadithi kutoka kwa Mtume- swala na salamu ziwe juu yake- kumekuja (hadithi) nyingi katika (kuelezea) kuwa waovu wengi waumini wataingia motoni na humo wataadhibiwa kwa kadri ya madhambi yao ,kisha watatoka humo (motoni),

ومنهم من يخرج بالشفاعة قبل أن يستوفي ما يستحقه من عقوبة،

na katika hao kuna yule atakayetoka kwa uombezi kabla ya kutimiza adhabu anayostahiki,

ومنهم من يغفر الله له بفضله ورحمته فلا يدخل النار.

na katika hao kuna yule (ambaye) Allah atamsamehe kwa fadhila zake na rehema zake hatoingia motoni,

▫️فأوصاف المسلمين ثلاثة أقسام:

Basi sifa za waislamu (zipo katika) vigawanyo vitatu :

١- قسم يغفر الله له ولا يدخل النار أصلاً.

1- (Kuna) kigawanyo (ambacho) Allah atakisamehe hakitoingia motoni kabisa .

٢-وقسم آخر يدخل النار ويعذب بقدر ذنوبه ثم يخرج.

2- Na kigawanyo kingine kitaingia motoni na kitaadhibiwa kadri ya madhambi yake kisha kitatoka .

٣-وقسم ثالث يدخل النار ويعذب ولكن يكون له الشفاعة فيخرج من النار قبل أن يستكمل ما يستحقه من العذاب. نعم.

3- Na kigawanyo cha tatu kitaingia motoni na kitaadhibiwa lakini kitakuwa na uombezi , basi (kigawanyo hiki) kitatoka motoni kabla ya kukamilisha kile kinachostahiki katika adhabu .

Ndio .

🔉فتاوى نور على الدرب الشريط رقم ( ٣٢٩)

Maelezo ya mtarjumu:

Huu ndiyo ubora wa tauhid na mtu wa tauhidi hatokaa motoni milele kwa maana mtu aliyefariki hali anamuabudia Allah pekee na wala hamshirikishi na chochote basi mtu huyo makazi yake ni peponi tu ,na
kumekuja hadithi nyingi zinazoonesha kuwa mtu aliyefariki hali hamshirikishi Allah -aliyetukuka- kwa maana aliyefariki hali ni muislamu asiyemshirikisha Allah wala kukufuru basi mtu huyo ukomo wake ni peponi na hata kama ataadhibiwa motoni kwa madhambi aliyoyafanya na akafa bila ya kutubu lakini atatolewa na kuingizwa peponi .

Amesema Mtume- swala na salamu zimfikie-:

لَيُصِيبَنَّ أقْوامًا سَفْعٌ مِنَ النَّارِ، بذُنُوبٍ أصابُوها عُقُوبَةً،

Kuna watu watapatwa na athari /joto la moto (ikiwa) ni adhabu kwa sababu ya madhambi waliyoyafanya,

ثُمَّ يُدْخِلُهُمُ اللَّهُ الجَنَّةَ بفَضْلِ رَحْمَتِهِ، يُقالُ لهمُ الجَهَنَّمِيُّونَ.

kisha (watatolewa na) Allah atawaingiza peponi kwa fadhila za huruma wake , (watu hao) wataitwa: Watu wa Jahannam .

رواه البخاريُّ

Mtarjumu:Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 10, 1443H ≈ November 15, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *