Hali ya wema waliopita katika kuwasaidia ndugu zao.

قال ابن كثير الشافعي -رحمه الله- رحمه الله- :

Amesema ibn Kathir Asshafiy – Allah amrahamu-:

كان يحيى بن خالد البرمكي يجري على سفيان بن عيينة كل شهر ألف درهم،

Alikuwa Yahy bin Said Al-Barmakiy akimpa Sufian bin ‘Uyainah kila mwezi dirhamu elfu moja,

وكان سفيان يدعو له في سجوده يقول:

Naye Sufiani alikuwa akimuombe dua (akiwa) amesujudu akisema (hivi):

اللهم إنه قد كفاني المؤنة وفرغني للعبادة فاكفه أمر آخرته.

Ewe Allah! hakika huyo (mja wako) amenitoshelezea gharama za maisha na akanifanya mimi nishughulike na ibada, basi mtoshelezee jambo la akhera yake .

فلما مات يحيى رآه بعض أصحابه في المنام فقال:

Basi Yahya alipofariki baadhi ya watu wake walimuona ndotoni na (walimuuliza) wakasema :

ما فعل الله بك؟

Allah amekufanyia nini ?

قال: غفر لي بدعاء سفيان.

(Yahya) akasema: “Amenisamehe na kunistiri kwa sababu ya dua ya Sufiani ” .

البداية والنهاية 677/13

Maelezo ya mfasiri:

Hivi ndivyo wema waliopita walivyokuwa wakiwasaidia ndugu zao katika imani na hivi ndivyo walivyokuwa wakichunga thamani ya undugu wao wa kiislamu ! kwa sababu wao walijua uzito wa ibada hii na utukufu wa malipo yake kama vile kupata msamaha wa Allah kwa kufutiwa madhambi kama ilivyotokea kwa huyu Yahya, na vilevile waliifanyia kazi kauli yake Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-:

وَاَللَّهُ فِي عَوْنِ الْعَبْدِ مَا كَانَ الْعَبْدُ فِي عَوْنِ أَخِيهِ،

“Na Allah humsaidia mja muda ambao mja humsaidie ndugu yake”

رواه مسلم

Na bila shaka mja anapomsaidia ndugu yake basi Allah -aliyetukuka- naye humsaidia na humkunjulia riziki yake na kumuwepesishia na ndiyo maana huyu Yahya -Allah amrahamu- alikuwa alikuwa ana uwezo wa kumpa Sufiani-Allah amrahamu- dirhamu elfu moja kila mwezi na haswa pindi anapokuwa yule anayesaidiwa ni mtu mwenye kushughulika na ibada ambayo manufaa yake ni yenye kuenea kwa jamii ya kiislamu kama vile kutafuta elimu au kuifundisha ,na hili lilitokea katika zama za Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie-

كانَ أخَوانِ على عَهْدِ النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ علَيهِ وسلَّمَ فَكانَ أحدُهُما يأتي النَّبيَّ صلَّى اللَّهُ علَيهِ وسلَّمَ والآخرُ يحترِفُ،

Kulikuwa na ndugu wawili katika zama za Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- alikuwa mmoja wao anakuja kwa Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- (kwa ajili ya kutafuta elimu) na (huyu) mwengine (alikuwa) akitafuta riziki

فشَكَى المحترفُ أخاهُ إلى النَّبيِّ صلَّى اللَّهُ علَيهِ وسلَّمَ

Basi yule anayefanya kazi akamshtakia ndugu yake kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-

فقالَ: لعلَّكَ ترزقُ بِهِ

basi Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- akasema (hivi) :

“Huwenda wewe (ukawa) unaruzukiwa kwa sababu yake ”.

رواه الترمذي

Ufafanuzi wa hadithi :

Kutafuta elimu ya dini na kuwasimamia wenye kutafuta elimu ya dini ni katika sababu za mtu kukunjuliwa riziki yake.

Tanbih:

Hadithi hii haina maana kwamba watu wabweteke na wasijitume katika kutafuta riziki, hapana bali watu wajitahidi katika kutafuta na wafanye kazi ,na wajizuie kuombaonba lakini yule ambaye Allah amemkunjulia riziki basi asijidai kwa kipato alichokuwa nacho kwa sababu hiyo riziki imetoka kwa Allah ,bali awasaidie ndugu zake wasiokuwa na uwezo

•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 29, 1445H =May 9, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *