Makala namba (1) .
🔺 قال العلامة العثيمين رحمه الله:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Uthaimin -Allah amrehemu-
▪️ القاعدة:
(كل من أخذ المال بغير حقه فإنه يبتلى بالشح كالذي يأكل ولا يشبع)، والذي يأكل ولا يشبع لا ينفعه أكله.
Kanuni:
Kila aliyechukua mali bila ya haki hakika (mtu) huyo atajaribiwa kwa uroho wa kupindukia (atakuwa) kama yule ambaye anayekula na wala hashibi.
Na yule ambaye anakula na wala hashibi kula kwake hakumnufaishi.
⏪ ولقد حدثنا أكابرنا سنّا أنه أتى على أهل نجد زمان يسمى سنة الجوع، يأكل الإنسان الأكل الكثير الذي لا يأكله الجمل،
Na hakika wametuhadithia wakubwa wetu kiumri kwamba kuna kipindi kiliwajia watu wa Najd kiliitwa mwaka wa njaa, mtu (alikuwa) anakula chakula kingi ambacho ngamia hawezi kukila,
بل أكثر مما يأكل الجمل نفسه، بالليل والنهار، ولكن لا يشبع أبدا، سبحان الله .
Bali (anakula) kingi zaidi kuliko anachokula ngamia mwenyewe, usiku na mchana lakini (mtu alikuwa) hashibi abadani- utakasifu ni wa Allah.
📚 التعليق على صحيح مسلم( 5 /191-192).
Maelezo ya mpitiaji:
Kuchuma mali kwa njia ya haramu ni sababu ya kuwa na uroho wa mali na kutotosheka na kuendelea kutafuta mali kwa pupa hata kwa njia za haramu ,kisha sheikh -Allah amrahamu- akamfananisha mtu huyu ni kama mtu ambaye anakula lakini hashibi ! kwa maana hanufaiki kula kwake na akataja tukio lililotokea katika sehemu za Najd katika mwaka ulioitwa ni mwaka wa njaa : Mtu alikuwa anakula sana lakini hashibi kwa maana huu ni mlipuko wa njaa ambao ulitokea sehemu hizo mtu alikuwa anakula lakini hashibi kwa maana chakula kipo kwa wingi lakini mtu akila hashibi kwa sababu ya maradhi ambayo Allah ameyakadiria katika miili yao ,kama alivyoeleza sheikh katika sehemu nyinge kama vile katika tafsiri yake ya suratul-balad.
Inaendelea -Allah akitaka-.
Mpitiaji : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 26, 1443H ≈ Dec 30, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•