HAYA YA MOLA MLEZI KWA MJA WAKE .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

قال ابن القيم – رحمه الله:

Amesema ibn l-Qayyim – Allah amrahamu-:

وأما حياء الرب تعالى من عبده:

فذاك نوع آخر، لا تدركه الأفهام، ولا تكيفه العقول، فإنه حياءٌ وكرم وبِرٌّ وجودٌ وجلال، فإنه تبارك وتعالى حييٌّ كريم يستحي من عبده إذا رفع إليه يديه أن يردهما صفرا، ويستحي أن يعذب ذا شيبة شابت في الإسلام.

Ama haya ya Mola mlezi kwa mja wake:

Hiyo ni (haya) ya aina nyingine (ambayo) fahamu (haiwezi) ikaizunguka na wala akili (haiwezi) ikaifahamu ilivyo, basi bila shaka hiyo ni haya na ukarimu na wema na utoaji na utukufu, basi bila shaka yeye (Allah) ni mwenye haya na ni mkarimu anamuonea haya mja wake atakaponyanyua mikono yake miwili kumuelekea (yeye Allah) kuirudisha patupu, na anamuonea haya kumuadhibu mwenye mvi aliyeota mvi (aliyezeeka) katika uislamu.

📚 مدارج السالكين (١٩٤/٢)

Maelezo:

Allah anasifa ya haya kwa ule ukarimu wake na wingi wake wa kutoa anaona haya kumrudisha mikono mitupu huyo muombaji aliyenyanyua mikono kwa kumuelekezea yeye, lakini si kama haya na aibu ya viumbe bali hii ni haya inayonasibiana na utukufu wake na ukamilifu wake Allah kama alivyosema mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-:

{ إِنَّ رَبَّكُمْ حَيِيٌّ كَرِيمٌ يَسْتَحِي مِنْ عَبْدِهِ إِذَا رَفَعَ يَدَيْهِ إِلَيْهِ أَنْ يَرُدَّهُمَا صِفْرًا }.

{ Bila shaka Allah ni mwenye haya na mkarimu anamuonea haya mja wake pindi ataponyanyua mikono yake kuelekea kwake airudishe patupu }.

Ama hadithi inayosema kuwa Allah anamuonea haya kumuadhibu aliyeota mvi katika uislamu hii ni dhaifu,

قال العلامة المعلمي- رحمه الله – في تعليقه على: { الفوائد المجموعة }

Amesema mwanachuoni mkubwa Al-mu’alimiy – Allah amrahamu – katika maelezo yake mafupi katika kitabu: { Al-fawaaidu l-maj’muu’ah } -alipotaja hadithi zinazozungumzia ubora wa mvi-.

( ص ٨٤٠ ): { كلها هباء }

(Ukurasa 780): { Zote ni mavumbi } -kwa maana si sahihi-.

ثم قال:

kisha akasema:

ويكفي في هذا الباب قول الله تبارك وتعالى: { والله لا يستحي من الحق }

Na inatosha katika huu mlango kauli ya Allah – aliyezidi heri na aliyetukuka- :

{ Na Allah haoni haya kutokana na haki }.

Maelezo:

Amesema imamu Al-Baghawiy – Allah amrahamu-:

أي: لا يترك تأديبكم وبيان الحق حياء.

Maana ya (hiyo aya): Haachi kukuadabisheni na kubainisha haki kwa (sababu ya) haya.

Kwa hiyo matendo mema ndiyo sababu ya kuokoka na adhabu za moto, pamoja na kuwa kumekuja dalili nyingi zinazoonesha ubora wa mzee katika uislamu katika hizo hadithi ni kauli yake Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-:

{ لا تَنْتِفوا الشَّيْبَ، فإِنه ما من مسلم يَشِيبُ شَيبة في الإسلام، إلا كانت له نوراً يوم القيامة }

{ Msizinyofoe mvi basi hakika hali ilivyo hakuna muislamu yeyote anayetokwa na mvi katika uislamu isipokuwa itakuwa ni nuru kwake siku ya kiama }

📚 رواه أبو داود وصححه الألباني.

Maelezo:

Uzee ambao kwa kawaida huambatana kutokwa na mvi katika uislamu kuna ubora,na katika huo ubora ni kuwa hizo mvi ni nuru katika giza la siku ya kiama na uzee ni sababu ya mtu kushikamana na ibada na kurudi kwa Allah.

Mfasiri: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Toleo la kwanza: 13/Dhul-hijjah – 1441H≠ 03-August-2020M ,Toleo la pili: Swafar/Mfungo tano 25 , 1443H ≈ Oct 2, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

  1. Bachu Ally

    السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *