Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
كنوز يوم عرفة
HAZINA ZA SIKU YA ARAFAH .
🤲🏻 أفضل أيام السنة للدعاء
Siku bora zaidi ya mwaka kwa kuomba dua
🔹 قَالَ رَسُولُ اللَّه ﷺ:
” خيرُ الدُّعاءِ دعاءُ يومِ عرفةَ، وخيرُ ما قلتُ أَنا والنَّبيُّونَ من قبلي:
👈🏻 لا إلَهَ إلَّا اللَّهُ وحدَهُ لا شريكَ لَهُ ، لَهُ الملكُ ولَهُ الحمدُ وَهوَ على كلِّ شَيءٍ قديرٌ “.
Amesema Mtume wa Allah- swala na salamu za Allah zimfikie- :
Dua bora zaidi ni dua ya siku ya Arafah ,na (maneno) bora zaidi niliyoyatamka mimi na manabii kabla yangu:
Hakuna muabudiwa anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah mpweke hana mshirika,ufalme wote ni wa kwake pekee ,na sifa njema zote ni za kwake pekee, naye juu ya kila kitu ni muweza “.
📚 حسنه الألباني في
صحيح الترمذي (٣٥٨٥)
💢 قال الإمام النووي الشَّافِعِيّ – رحمه الله:
Amesema imamu Nnawawiy Asshaafi’iy- Allah amrahamu-:
👈🏻 فهذا اليوم أفضل أيام السنة للدعاء، فينبغي أن يستفرغ الإنسان وسعه في الذكر والدعاء وقراءة القرآن،
Basi hii siku (ya Arafah) ni siku bora zaidi ya mwaka kwa kuomba dua,basi inatakikana mwanadamu atoe juhudi zake katika (kuleta) nyiradi na kuomba dua na kusoma qurani,
وأن يدعو بأنواع الأدعية ويأتي بأنواع الأذكار، ويدعو لنفسه ووالديه وأقاربه ومشايخه وأصحابه وأصدقائه وأحبابه وسائر من أحسن إليه وجميع المسلمين.
na aombe aina mbalimbali za dua na alete aina mbalimbali za nyiradi ,na ajiombee mwenyewe, na wazazi wake wawili na ndugu zake na mashekhe zake na watu aliokuwa nao, maswahibu zake, na rafiki zake , na vipenzi vyake ,na wote waliomfanyia wema, na waislamu wote .
👌 وليحذر كل الحذر من التقصير في ذلك كله، فإن هذا اليوم لا يمكن تداركه.
na (muislamu) awe na tahadhari mno kuzembea katika yote hayo ,na bila shaka siku hii haiwezekani kurekebishwa (utakapoiharibu).
📙 كتاب الأذكار للنووي طبعة دار المنهاج ص (٣٣٣)
💢 قال الحافظ ابن عبد البر المالكي – رحمه الله:
Amesema Al-hafidh bin ‘Abdil-Barr Al-maalikiy -Allah amrahamu-:
👈🏻 وفيه من الفقه أن دعاء يوم عرفة أفضل من غيره، وفي ذلك دليل على فضل يوم عرفة على غيره،
Na ndani ya (hadithi) hiyo kuna elimu (tunaipata nayo ni) : kuwa dua ya siku ya Arafah ni bora zaidi ya siku nyingine ,na katika hilo kuna dalili juu ya ubora wa siku ya Arafah juu ya siku nyingine,
👌وفي الحديث أيضًا دليل على أن دعاء يوم عرفة مجاب كله في الأغلب.
na katika hadithi (hii) pia kuna dalili juu ya kuwa dua za siku ya Arafah ni zenye kujibiwa zote mara nyingi .
📕 التمهيد (٦/ ٤١)
Maelezo ya mfasiri:
Jipinde kuomba dua katika siku hii tukufu kwa kutaraji kujibiwa na jipinde kwa ibada mbalimbali , haswa baada ya swala ya adhuhr na haswa kabisa baada ya Alasiri mpaka kuzama kwa jua ,na kama mtu akifunga siku hii aombe dua pia wakati anapofuturu kwa sababu dua wakati huo ipo karibu zaidi na kujibiwa , pia katika siku hii ya Arafah tukithirishe kutamka tamko la tauhidi kwa kutafuta radhi za Allah na kwa ukweli unaotoka katika nyoyo zetu , kumbuka siku hii ukiikosa mwaka huu hujui kama mwakani utakuwa bado katika mgongo wa ardhi au kaburini !.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 9 siku ya Arafah, 1442H ≈ Jul 19, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•