HEKIMA YA KUIGAWA NYAMA YA UDH’HIYAH MAFUNGU MATATU .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

ما الحكمة من تقسيم الأضحية ثلاثا.

IPI HEKIMA YA KUIGAWA (NYAMA YA) UDH’HIYAH (MAFUNGU) MATATU ?

قال العلامة ابن عثيمين - رحمه الله: 

Amesema mwanachuoni mkubwa Ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu:

حتى يجتمع في الأضحية ثلاثة أمور مقصودة شرعية:

Ili kukusanyike katika udh’hiyah, mambo matatu yanayo kusudiwa kisheria (nayo ni):

الأول: التمتع بنعمة الله وذلك في الأكل منها.

الثاني: رجاء ثواب الله وذلك بالصدقة منها.

1 -(jambo) la kwanza:
Ni kustarehe kwa neema za Allah, na hilo ni kwa kula katika hiyo (udh’hiyah),

2 – (jambo) la pili: Kutaraji thawabu (malipo) na hilo ni kwa kutoa sadaka,

الثالث: التودّد إلى عباد الله وذلك بالهدية منها.

3 – (jambo) la tatu:Kujipendekeza kwa waja wa Allah na hilo ni kwa kutoa zawadi katika hiyo (udh’hiyah),

وهذه معان جليلة مقصودة للشرع،
ولهذا استحب بعض العلماء أن تكون أثلاثا:

فثلث يأكله،
وثلث يتصدق به،
وثلث يهديه.

Na hizi ni maana mzuri zinazokusudiwa na sheria,

Kwa ajili hii wamependekeza baadhi ya wanachuoni (udh’hiyah) iwe sehemu tatu:

Theluthi moja atakula (mwenyewe),

na theluthi (ya pili) anaitoa sadaka,

na theluthi (ya tatu) ataitoa zawadi.

📚 المصدر: مجموع الفتاوى (٢٥/١٤)
[ Maj’muu’u l-fataawaa (14/25) ]

Maelezo na faida kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi

Hii ni moja ya fatwa ya sheikh – Allah amrahamu – katika kugawa mafungu ya nyama ya udh’hiyah nayo ni kuigawa mafungu matatu :

1- Fungo moja ale mwenyewe .

2- Fungi la pili alitoe sadaka .

3- Fungu la tatu alitoe zawadi , na hii ndiyo kauli inayotegemewa katika madhehebu (ya kishafii) ,

na sheikh anafatwa nyingine inayoeleza kuwa hakuna dalili au hoja ya kuigawa mafungu matatu, bali ni mapendekezo ya baadhi ya wanachuoni,

kinachotakiwa ni kugawa sehemu ya nyama na wala usile peke yako unaweza ukagawa mafungu mawili unaweza ukagawa kidogo au nyingi hakuna kiwango maalumu na hii ni kauli ya sheikh Al-baniy – Allah amrahamu – , na katika kugawa kwako usiwasahau mafakiri na mafukara katika waislamu wenzako.

Chakuzingatia ni kuwa usile nyama yote peke yako ni lazima utoe sehemu japo kidogo uwape mafakiri /masikini, hiki ndicho kiwango cha wajibu cha kutoa katika nyama ya udh’hiyah .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Iliandaliwa: August 10, 2019M ikarushwa tena Dhul-Qaadah 30, 1442H ≈ Jul 10, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

  1. Abu Muhammad Sadiki

    Mdaiwa (mwenye Deni) anapaswa kutia nia ya kuchinja, baarakallahu fikhi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *