Heri za dunia na ahera zipo katika haya!

‏قال الإمام الشافعي رحمه الله :

Amesema imamu Shafii- Allah amrahamu-:

خيرُ الدنيا والآخرة في خمسِ خِصال :

Heri za dunia na ahera zipo katika mambo matano:

غِنى النفس، وكف الأذى، وكسب الحلال،ولباسِ التقوى، والثقةِ بالله تعالى على كل حال.

Utajiri wa nafsi (kutosheka), na kujizuia na maudhi, na kuchuma (chumo) la halali, na (kuvaa) nguo ya uchamungu, na kuwa na tumaini kwa Allah aliyetukuka juu ya kila hali .

📚 بستان العارفين (ص١٥٩).

Maelezo ya mfasiri:

Anatuambia imamu wetu Shafi-Allah amrehamu-kuwa kheri za dunia na akhera zipo katika matano haya :

Jambo la kwanza :

Kutosheka na kile ulichoruzukiwa na Allah katika dunia na bila shaka kutosheka ni katika sababu za mtu kuishi maisha yenye raha na kupata heshima kwa watu, na huo ndiyo utajiri wa kweli kama alivyosema Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – pale aliposema:

” ليسَ الغنى عن كثرةِ العَرَضِ ولَكنَّ الغِنى غنى النَّفسِ“

“ Utajiri hautokani na wingi wa mali lakini utajiri ni utajiri wa nafsi (kutosheka)”

متفق عليه.

Kuna mashairi iliyoyaandika pia huyu imam Shafiy -Allah amrahamu- yanayojulisha ubora wa kuwa na kanaa yaani kutosheka, pale aliposema:

رَأَيتُ القَناعَةَ رَأسَ الغِنى
فَصِرتُ بِأَذيالِها مُمْتَسِكْ

Nimeona kutosheka ndiyo msingi wa utajiri, basi nikakamatia kamba zake sawa sawa

فَلا ذا يَراني عَلى بابِهِ
وَلا ذا يَراني بِهِ مُنهَمِكْ

Basi yule hanioni mlangoni kwake (nikimuomba) , na wala hanioni nikimtilia umuhimu .

فَصِرتُ غَنيًّا بِلا دِرهَمٍ
أَمُرُّ عَلى الناسِ شِبهَ المَلِكْ

Basi nimekuwa tajiri bila ya dirham (pesa), napita kwa watu mfano wa mfalme .

Jambo la pili:

Kujizuia na kuwaudhi watu

Bila shaka kumethibiti hadithi nyingi zinazoenesha ubora wa kujizuia kuwaudhi watu na ubora wa kuondoa maudhi kwa watu, na miongoni mwa hadithi hizo ni hadithi inayosimuliwa na Abuu Dharr – Allah amridhie-ambayo ndani yake Abu Dharr alimuuliza mtume -rehema na amani za Allah zimfikie – maswali kadhaa yanayohusu ubora wa baadhi ya ibada na baada ya kujibiwa akamwambia Mtume- rehema na amani za Allah zimfikie – maneno yafuatayo:

يَا رَسُولَ اللهِ، أَرَأَيْتَ إِنْ ضَعُفْتُ عَنْ بَعْضِ الْعَمَلِ؟

Ewe mtume wa Allah! nielezee kama nikidhoofika nikashindwa (kufanya) baadhi ya matendo, (nifanye nini) ?

قَالَ: «تَكُفُّ شَرَّكَ عَنِ النَّاسِ فَإِنَّهَا صَدَقَةٌ مِنْكَ عَلَى نَفْسِكَ»

Akasema (Mtume) – rehema na amani za Allah zimfikie -:

“ Zizuie shari zako kwa watu hakika (kufanya) hivyo ni sadaka unayojitolea mwenyewe ”

متفق عليه.

Jambo la tatu:

Kutafuta riziki ya halali :

Kufanya kazi kwa kuchuma chumo halali hii ilikuwa ni kawaida ya watu wema kuanzia manabii na wafuasi wao kama anavyoeleza Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – :

” ما أكلَ أحدٌ طعامًا قطُّ ، خيرًا من أنْ يأكلَ من عمَلِ يدِهِ وإنَّ نبيَّ اللهِ داودَ كان يأكلُ من عمَلِ يدِهِ“

” Hajapatapo mtu kula chakula kilichokuwa bora katu kuliko kula kwa chumo la mikono yake, na hakika nabii wa Allah Daud alikuwa akila kwa kazi ya mikono yake ”

متفق عليه.

Ufafanuzi wa hadithi:

Ndani ya hadithi hii kuna himizo la watu kufanya kazi ya halali na kula kwa jasho lao na wala haifai mtu kuwa mzigo Kwa wengine kwa kuombaomba, na kufanya kazi kwa ajili ya kupata riziki ya halali ni kawaida ya watu wema kuanzia manabii na wafuasi wao kama tulivyoeleza hapo juu .

Jambo la nne:

Kujipamba na vazi la uchamungu:

Kama alivyosema Allah -aliyetukuka- katika kitabu chake kitukufu:

﴿ يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنْزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ وَرِيشًا وَلِبَاسُ التَّقْوَى ذَلِكَ خَيْرٌ ذَلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ ﴾

Enyi wanadamu! Hakika tumekuteremshieni nguo zinazoficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za uchamungu ndizo bora .Hayo ni katika ishara za (neema za) Allah ili wapate kukumbuka .

سورة الأعراف ٢٦

Ufafanuzi wa aya :

Katika aya hii Allah -aliyetukuka-anawatajia wanadamu miongoni mwa neema alizowapa nayo ni neema ya kuwapa nguo /mavazi ya kustiri tupu zao na akawapa ziada ya mavazi ya mapambo lakini akasema kuwa nguo ya uchamungu ni bora kwa maana mtu kujipamba na imani na matendo mema na kujiepusha na maovu na kumuogopa Allah hili ni vazi bora na pambo zuri kwao.

Jambo la tano:

Kuwa na tumaini kwa Allah juu ya kila hali :

Maana ya kuwa na matumaini kwa Allah : Ni kuwa na yakini madhubuti kuwa Allah amekamilika kwa sifa za utukufu na uzuri na ukweli wa ahadi zake, na ukubwa wa uwezo wake na elimu yake imezunguka kila kitu.

Bila shaka yule mwenye kuwa na tumaini kwa Allah hatomuogopa kiumbe na wala hatotaraji kutoka kwake na hatouza dini yake kwa kutafuta dunia kwa sababu yeye anajua kuwa ayetegemewa katika mambo yote ni Allah pekee na yeye ndiye mmiliki wa kila kitu .

{ وَمَنْ يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ}

Na anayemtegemea Allah (basi) yeye Allah humtosheleza .

سورة الطلاق.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nne 12, 1446H ≈ Jul /18, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *