HII NDIYO DUNIA !

🎙️قال العلامة ابن الجوزي رحمه الله تعالى-:

Amesema mwanawachuoni mkubwa ibn l-Jauziy -Allah aliyetukuka amrahamu-:

✍️ “واعلم أن الزمان لا يثبت على حال، قال عز وجل:

Tambua kuwa zama hazithibiti katika hali (moja), amesema (Allah) aliyeshinda na kutukuka:

﴿ وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ﴾

Na siku za namna hii tunawaletea watu kwa zamu .

فتارة فقر، وتارة غنى، وتارة عز، وتارة ذل ،وتارة يفرح الموالي، وتارة يشمت الأعادي،

Basi (hii dunia) wakati mwingine (huwa) ni ufakiri na wakati mwingine ni utajiri na wakati mwingine ni utukufu na wakati mwingine ni udhalili na wakati mwingine wanafurahi wanaokupenda na wakati mwingine wanafurahi maadui zako

فالسعيد من لازم أصلًا واحدًا على كل حال، وهو تقوى الله عز وجل فإنه إن استغنى زانته، وإن افتقر فتحت له أبواب الصبر،

Basi mtu mwema ni yule aliyejilazimisha na msingi mmoja katika kila hali, nao ni (msingi wa) kumcha Allah -aliyeshinda na kutukuka bila shaka huo (msingi):

Kama (mtu) akiwa tajiri utampamba, na kama akiwa fakiri utamfungulia milango ya subira

وإن عوفي تمت النعمة عليه، وإن ابتلي حملته،

na kama akipewa afya njema (basi) neema hutimia kwake ,na kama akipewa mtihani humbeba ,

ولا يضره إن نزل به الزمان أو صعد، أو أعراه أو أشبعه أو أجاعه؛

Na wala hakuna kitakachomdhuru kama zama zitamshusha au kumpandisha au zikamweka uchi au zikamshibisha au zikampa njaa

لأن جميع تلك الأشياء تزول وتتغير، والتقوى أصل السلامة حارس لا ينام”.

Kwa sababu vitu vyote hivyo huondoka na kubadilika na ucha Mungu ndiyo msingi wa kusalimika (na) ni mlinzi asiyelala .

📚 المصدر: صيد الخاطر ٣٩/١

Maelezo ya mfasiri:

Tupo katika dunia na hizi siku Allah huzigeuza kati ya watu: Wakati mwengine hali hii wakati mwengine hali hii zama hazidumu katika hali moja silaha pekee ni ucha Mungu tu .

Tambua kuwa katika hii dunia ni lazima Allah atakujaribu kwa mitihani mbalimbali kama alivyosema mshairi:

ثَمَانِيَةٌ تَجرِي عَلَى النَّاسِ كُلِّهِم
وَلا بُدَّ لِلإِنسَانِ يَلقَى الثَّمَانِيَهْ

(Mambo) manane huwapitia watu wote, hakuna budi kwa mwanadamu akutane na (mambo) manane .

سُرُورٌ وَحُزنٌ وَاجتِمَاعٌ وَفُرقَةٌ
وَيُسرٌ وَعُسرٌ ثُمَّ سُقمٌ وَعَافِيَه

Furaha, na huzuni , na kuwa pamoja , na kutengana, na wepesi,na uzito kisha maradhi na afya .

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 9, 1445H ≈ Oct/12, 2024M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *