HII NDIYO HALI YA MWANADAMU MPAKA KIAMA .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

HII NDIYO HALI YA MWANADAMU MPAKA KIAMA !

قَـالَ اللهُ عَــزْ وجَــلْ -:

{لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقࣲ}

(الانشقاق :١٩)

Amesema Allah -aliyeshinda na kutukuka-:

{Lazima mutakutana na tabaka ( hali) baada ya tabaka (hali)} .

(Surat al-inshiqaaq :19)

✅ قال ابن القيم رحمه الله :

Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:

👈🏻 أي حالا بعد حال!
🔷 فأول أطباقه: كونه نُطفة، ثم علقة، ثم مُضغة، ثم جنينًا، ثم مولودًا، ثم رضيعًا، ثم فطيمًا،

Maana yake : Hali baada ya hali ,na mwanzo wa matabaka (hali) zake (anazozipitia mwanadamu) : Kuwa kwake manii ,kisha pande la damu kisha pande la nyama kisha kitoto (tumboni) ,kisha kitoto kilichozaliwa ,kisha kitoto chenye kunyonya ,kisha mwenye kuacha kunyonya ,

ثم صحيحًا أو مريضًا، غنيًا أو فقيرًا، معافى أو مبتلى- إلى جميع أحوال الإنسان المختلفة عليه إلى أن يموت.

kisha (ima) mzima au mgonjwa ,tajiri au masikini ,aliyekingwa na mabalaa au aliyejaribiwa – (zinaingia) hali zote za mwanadamu tofauti tofauti (zinazotokea) juu yake mpaka atapofariki .

↩️ ثم يُبعث، ثم يوقف بين يدي الله، ثم يصير الى الجنة أو النار.
🔻 فالمعنى: لتركبنَّ حالاً بعد حالٍ، ومنزلاً بعد منزلٍ، وأمرًا بعد أمرٍ.

kisha atafufuliwa ,kisha atasimamishwa mbele ya Allah ,kisha (ima) ataelekea peponi au motoni .

Basi maana (ya aya hii) :

Lazima mutakutana na hali baada ya hali ,daraja baada ya daraja ,jambo baada ya jambo .

📚 تحفة المودود بأحكام المولود – ابن_القيم

Maelezo ya mfasiri :

Mwanadamu anahama na kubadilika kutoka katika hali moja kwenda hali nyingine kama alivyotaja sheikh -Allah amrahamu- na pia :

Mwanadamu kuna siku huwa na furaha na siku nyingine huwa na huzuni kama alivyosema mshairi :

فيومٌ علينا ويومٌ لنا ،،، ويومٌ نساءُ ويومٌ نُسرْ

(kuna) siku tunapata mabalaa na kuna siku tanapata raha ..

..kuna siku tunaudhiwa na kuna siku tunafurahishwa .

basi hii ndiyo hali ya mwanadamu ,baadhi ya nyakati huwa na khofu na baadhi ya siku huwa na amani ,ukame ,mvua , na hali nyingine mbali mbali ambazo hupitia mwanadamu mpaka pale atapofikiwa na kifo kisha kuzikwa na kuwa kaburini kisha kufufuliwa kisha ima peponi au motoni .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 20, 1442H ≈ Jun 1, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *