HILI NDILO LILILOTUANGAMIZA

‏كان الصحابي حكيم بن حزام
-رضي اللّه عنه- من أشراف قريش

Alikuwa swahaba Hakimu bin Hizam -Allah amridhie -ni katika watukufu wa Kikuraishi

وكان يطلب العلم عند الصحابي معاذ بن جبل -رضي اللّه عنه-

Na alikuwa akitafuta elimu kwa swahaba Muadhi bin Jabal -Allah amridhie –

رغم أنه كان أكبر من معاذ بخمسين سنة!

pamoja na kuwa yeye alikuwa ni mkubwa kuliko Muadhi kwa miaka hamsini!

فقيل له:

(kuna siku) aliambiwa :

أنت تتعلم على يد هذا الغلام؟!
فقال: إنما أهلكنا التكبر !

Hivi wewe unajifundisha kwa huyu kijana mdogo ?!

Akajibu : Hakika si vinginevyo kimetuangamiza kiburi !

الآداب الشرعية لابن مفلح (٢/٢١٥)

Maelezo ya mfasiri :

Amesema kweli -Allah amridhie -miongoni mwa sababu zinazomzuia mtu kutafuta elimu ni kiburi, kama alivyosema mmoja katika wema waliopitia :

” اثنان لا يتعلمان، المستحي والمتكبر “

“ (Watu wa) aina mbili hawatojifundisha mwenye kuona haya na mwenye kiburi ” .

Mwenye kiburi hawezi akapiga goti na kusoma kwa yule anayemdharau ima kwa umri wake mdogo au kwa udhalili wake au kwa kutokuwa na cheo nafasi, na madhara ya kiburi ni kufa na ujinga na kujifanya unajua kumbe hujui.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 13, 1443H ≈ Jun 13, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *