ذَكَرَ العلامة محمد الباقر المجلسي بالفارسية ما ترجمته بالعربية :
Ametaja mwanachuoni mkubwa(wa kishia) Muhammad Al-Baqir Al-majlisiy kwa (lugha) ya kifursi maneno ambayo tarjama yake kwa kiarabu (ni hivi) :
(أَنَّ أَبَا بَكْرٍ وَعُمَرَ هُمَا : فِرْعَوْنُ وَهَامَانُ )
Kwamba Abuu Bakr na Umar hao ni Firauni na Hamana .
حق اليقين للمجلسي ص ٣٦٧
Maelezo ya mfasiri:
Hivi karibuni kuna mmoja katika masheikh wa kishia alijaribu kutangaza donge nono la shilingi milioni tano kwa yeyote atakayeleta maneno ya yoyote katika kitabu cha mwanachuoni tegemezi wa kishia kilichotaja kuwa Abuu Bakr na Umar-Allah awaridhie-kuwa wamelaaniwa !.
Lakini lakusitikisha baada ya kupewa maneno hayo kutoka katika vitabu vyao vya wanachuoni wakubwa hawakutekeleza lile walilolitangaza bali wamebakia kuzungumza maneno ya kuwababaisha waislamu wasiojitambua !
Ndugu yangu muislamu:
Hapo juu tumewaletea maneno kutoka katika miongoni mwa vitabu vyao tegemezi na mwanachuoni wao tegemezi yanayosema kuwa:
“Abuu Bakr ni Firauni na Umar ni Hamana” , hivi ikiwa wanaitikadi kuwa Abuu Bakr ni Firauni na Umar ni Hamana ambaye alikuwa ni msaidizi wa Firauni ,na wote tunajua kuwa Firauni ni katika watu waliofikia ukomo katika uovu mpaka akadai uungu ! .
Ikiwa ni hivi basi, je hawa Mashia wanakusudia nini kama si kuzichezea akili za watu ! Ikiwa nyinyi mmemkufurisha Abuu Bakr na Umar tena mukasema kuwa wawili hao ni Firauni na Hamana kisha munawaomba Ahlu-sunnah walete maneno yenye kuwalaani kutoka kwa wanachuoni wenu tegemezi !
Hivi kumkufurisha mtu tena na kumpa daraja la Firauni na Hamana ni dogo hili kuliko kumlaani ?!.
Mwandishi : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Imeandaliwa : 26/Mfungo tisa/1444H- Jan/19/2023M
Tembelea Chanel yetu: ☟
https://t.me/Majmuutulaabifiqhishafii
Group la WhatsApp:☟
https://chat.whatsapp.com/LCmiCMbfYC2BHFpca0NFy2
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•