HOFU YA (KUPATA) MWISHO MBAYA !

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

الخوف من سوء الخاتمة

Hofu ya (kupata ) mwisho mbaya

لقد بكى سفيان الثوري ليلةً إلى الصباح ، فلما أصبح قيل له :

كلُّ هذا خوفاً من الذنوب ؟
فأخذ تِبْنةً من الأرض ،

Hakika Sufiyani bin Athauriy alilia usiku wote mpaka asubuhi,kulipokucha aliulizwa:

(kilio) chote hiki ni kwa kuogopa dhambi?

basi akachukua nyasi ardhini,

وقال :
الذنوب أهون من هذا ، وإنما أبكي من خوف الخاتمة.

na akasema: Dhambi ni nyepesi zaidi kuliko hizi (nyasi) , hakika sivinginenvyo nalia kwa kuchelea mwisho mbaya.

قال ابن القيم رحمه الله :

Akasema ibn Al-qayyim -Allah amrehemu- (akifafanua):

وهذا من أعظم الفقه : أن يخاف الرجل أن تخذله ذنوبه عند الموت ، فتحول بينه وبين الخاتمة بالحسنى .

Na huu ndio ufahamu mkubwa zaidi .Mtu akachelea madhambi yake yakawa ni sababu ya kutoafikishwa wakati wa kufa,(na) yakawa ni kizuizi baina yake na baina ya mwisho mwema.

[ الداء والدواء صـ٣٩٠ ]

Maelezo ya mpitiaji:

Bila shaka kila muislamu anamuomba Allah -aliyetukuka- ampe taufiki ya kuupata mwisho mwema na anamuomba Allah amkinge na mwisho mbaya na hivi ndivyo walivyokuwa wema waliopita walikuwa hawaziaminishi nafsi zao bali walikuwa wakimlilia Allah -aliyetukuka- awaepushe na mwisho mbaya pamoja na ibada nyingi walizokuwa nazo .

Na sababu ya kupata mwisho mbaya ni kufanya maovu na kuyapenda maovu na kuendelea nayo .

قال الشيخ صديق حسن خان -رحمه الله-:

Amesema sheikh Swiddiq Hasan Khan -Allah amrahamu- :

“فطول الإِلْف بالمعاصي يقتضي تذكُّرها عند الموت،

Kozoea (kufanya) maasi kwa muda mrefu hupelekea kuyakumbuka wakati wa kifo,

وعودها في القلب وتمثُّلها فيه، وميل النفس إليها،

na hujirudia katika moyo na huleta picha katika (moyo) ,na nafsi huyaegemea

وإن قُبض روحه في تلك الحالة يختم له بالسوء”؛ اهـ.

na kama roho yake itatolewa katika hali hiyo hupewa mwisho mbaya .

يقظة أولي الاعتبار (ص ٢٠٥) .

Maana ya maneno ya sheikh : Mtu anapofanya madhambi muda mrefu matokeo yake ni kuyazoea hayo madhambi ni mtu pale anapokata roho huyakumbuka kwa sababu mtu anapokata roho hukikumbuka kile kitu anachokipenda na kilichoganda katika moyo wake ,na pia huja picha ya hayo maovu, na pia mtu anapozoea madhambi na nafsi yake pia huegemea katika hayo maovu na kama mtu atakufa katika hali hiyo basi anaweza akafa katika hali mbaya .

Na pia katika sababu za kupata mwisho mbaya ni mtu kufanya matendo mema kwa udhahiri lakini moyo wake ukawa na shari kama vile makusudio mabaya: watu wamuone, au akawa ni mnafiki n.k .

Imepitiwa na : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Muharram/Mfungo nne 6, 1443H ≈ September 13, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *