Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
سئل العلامة العباد- حفظه الله-:
Aliulizwa mwanachuoni mkubwa Al-‘abbaad- Allah amuhifadhi-:
هل تجزئ الحامل من بهيمة الأنعام في الأضحية؟
Je anatosheleza katika udh’hiyah (kuchinjwa) mwenye mimba katika wanyama wafugwao ?
الجواب:
Jawabu:
تجزئ الحامل، ولكن الأولى أن تجتنب.
Mwenye mimba anatosheleza/anafaa ,lakini bora zaidi ni kujiepusha naye (atafutwe mwingine) .
شرح سنن أبي داودللعباد (٣٣١/٣١)
Maelezo ya mfasiri:
Kuchinja udh’hiya mnyama mwenye mimba wanachuoni wengi zaidi wanaona inafaa ,lakini sheikh -Allah amuhifadhi- amesema inapendeza zaidi kutochinja mnyama mwenye mimba na hilo ni kwa sababu madhehebu (ya kishafi) yanasema haifai kuchinja udh’hiyah mnyama mwenye mimba kwa sababu mimba huaribu ndani ya tumbo la mnyama na huifanya nyama yake kuwa mbaya.
Ndio maana sheikh amejibu ni vizuri kujiepusha naye kwa sababu msingi wa kisheria unasema :
الْخُرُوْجُ مِنَ الْخِلَافِ مُسْتَحَبٌّ
Kujitoa katika tofauti (za wanachuoni) inapendeza.
Nyongeza :
Kama atamchinja mnyama mwenye mimba na mtoto akatoka tumboni hali ya kuwa amekufa basi huyo mtoto analiwa kwa hadithi ya Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- :
(ذَكَاةُ الْجَنِينِ ذَكَاةُ أُمِّهِ)
{Chinjo la kitoto (tumboni) ni chinjo la mama yake}
رواه ابن ماجه في سنن .
Mchanganuo:
Katika madhehebu (ya kishafi) kikiwa hicho kitoto kimetoka hali ya kuwa kipo hai lakini uhai wenyewe si uhai wa kutulizana mfano akawa hatingitishi na wala hajipigipigi , basi huyu pia akifa ataliwa ,ama kikizaliwa kitoto na kikakutwa na uhai uliotulizana na kikabakia hivyo mpaka kikafa bila ya kuchinjwa basi kitakuwa hakifai kuliwa .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 4, 1442H ≈ Jul 14,, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•