HUKUMU YA KUFUKIA NYWELE NA KUCHA BAADA YA KUZIKATA.

لسماحة الشيخ العلامة عبد العزيز ابن باز رحمه الله

(Fatwa) ya shekh mwanachuoni mkubwa Abdul-Aziz bin Baaz- Allah amrehemu-:

📌 السؤال رقم – ٤٩ : ﻫﻞ ﻳﺠﺐ ﺩﻓﻦ اﻟﺸﻌﺮ اﻟﻤﺘﺴﺎﻗﻂ، ﻭاﻷﻇﺎﻓﺮ اﻟﻤﻘﺼﻮﺻﺔ ﻓﻲ اﻟﺘﺮاﺏ ؟

Swali namba 49:

Je ni lazima kuzifukia chini nywele zinazokatika ,na kucha zilizokatwa?

✅ الجواب : ﻟﻴﺲ ﺑﻼﺯﻡ، ﻳﻠﻘﻴﻬﺎ ﻓﻲ اﻟﻘﻤﺎﻣﺔ، ﻭاﻟﺤﻤﺪ ﻟﻠﻪ، ﻣﺎ ﻓﻴﻪ ﺩﻟﻴﻞ ﻋﻠﻰ ﺩﻓﻨﻬﺎ، ﺇﺫا ﺃﻟﻘﺎﻫﺎ ﻓﻲ اﻟﻘﻤﺎﻣﺔ ﻛﻔﻰ، ﻭاﻟﺤﻤﺪ ﻟﻠﻪ.

Jawabu:

Sio lazima, (bali) atazitupa kwenye takataka -na sifa zote njema ni za Allah- ,hakuna dalili juu ya kuzifukia , akizitupa kwenye takataka yatosha,-na sifa zote njema ni za Allah.

📚 المصدر : فتاوى نور على الدرب (٥/٥٩)

Maelezo ya mpitiaji:

Na waliulizwa wanachuoni wa jopo la kudumu la utoaji fatwa la Saudia, na je ni haramu kuzitupa kucha baada ya kuzikata na inawajibika kuzifukia ?

Wakajibu:

يشرع تقليم الأظافر ، لأن إزالتها من خصال الفطرة ولا حرج في رميها ولا يجب دفنها فإن ألقاها في الزبالة أو دفنها فلا بأس بذلك .

Ni sheria kukata kucha kwa sababu kuziondoa (kucha) ni katika mambo ya kimaumbile na wala si vibaya na wala haiwajibiki kuzifukia ,kama atazitupa katika jalala au akazifukia basi hakuna ubaya wa hilo.

فتاوى اللجنة الدائمة ١٧٦/٥

Baadhi ya wanachuoni wa fiqih wanaona ni suna kuzifukia kucha na nywele zilizonyolewa nayo ni madhehebu ya Hanafiyah na Shafi, na Hanabilah, yafuatayo ni maneno ya baadhi ya wanachuoni wa fiqih:

قال النووي في المجموع (٣٤٢/١):

Amesema Annawawiy katika Al-maj’mu’u (1/342):

“يستحب دفن ما أخذ من هذه الشعور والأظفار، ومواراته في الأرض،

Ni suna kuzifukia nywele zilizokatwa na kucha na kuzificha katika ardhi,

نقل ذلك عن ابن عمر رضي الله عنهما، واتفق عليه أصحابنا”،

limenukuliwa hilo kutoka kwa ibn Umar-Allah amridhie- na wameafikiana juu ya hilo watu wetu /wanachuoni wa kishafii”

وانظر حاشية البجيرمي على الخطيب (٢٠٨/٢).

na yafuatayo ni maneno ya ibn Qudamah-Allah amrahamu- katika Mahanabila:

قال ابن قدامة في المغني (٦٤/١):

Amesema ibn Qudamah katika Al-mugh’n (1/64)

“ويستحب دفن ما قلم من أظفاره أو أزال من شعره…

“Ni suna (Mtu)kufukia kucha alizozikata au nywele zake alizozinyoa…

وانظر كشاف القناع (٧٦/١)، ومطالب أولي النهى (٨٧/١).

Mwisho:

Kwa hiyo kama itawepesika basi ni vizuri zaidi na bora zaidi kuzifukia kama ulivyoona maneno ya wanavyuoni na hata sheikh ibn Uthaimin-Allah amrahamu- ameiashiria kauli hii.

Mpitiaji : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 5, 1443H ≈ Dec 9, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *