قال العلامة ابن حجر الهيتمي -رحمه الله-:
Amesema mwanachuoni mkubwa ibn Hajar Al-haitamiy -Allah amrahamu -:
(ومحلُّ ذلك – أي: كراهة الإفراد – ما إذا لم يوافق إفراد كلٍ من الأيام الثلاثة – الجمعة والسبت والأحد – عادةً له، وإلا فلا كراهة)
Na mahali pa huo -yaani ukaraha wa kuzipwekesha -kama huko kuzipwekesha siku hizo tatu -Ijumaa, Jumamosi Jumapili hakukuafikiana na mazoea yake na kama (kukiafikiana) basi hakuna ukaraha
المنهج القويم ٤٢٠
Maelezo ya mfasiri:
Ijumaa au Jumamosi ikiafikiana na funga yake ya ada/mazoea kama vile funga ya Arafah kutakuwa hakuna ukaraha wa kuipwekesha siku hiyo kwa funga .
Na ukaraha wa kuzifunga siku hizi kwa kuzipwekesha unaondoka kama funga hiyo itaafikiana na ada na mazoea yake kama vile Arafah ikiangukia Ijumaa au Jumamosi, au kama aliweka nadhiri na ikaangukia siku ya Ijumaa au Jumamosi au kama analipa funga ya faradhi katika hali hizi zote ukaraha unaondoka, na pia kama yote hayo hayapo kwake ukaraha unaondoka kwa kufunga siku nyingine pamoja na siku hiyo kama vile akafunga Al-khamisi na Ijumaa .
Maelezo haya ameyatoa ibn Hajar -Allah amrahamu -katika kitabu chake kingine tuhfatul-muhtaj
Abuu Thurayyaa Ismail seiph Mbonde Asshaafi’y
حفظه الله تعالى ورعاه ووفقه
📚 العلم حیاة القلب📚
8- Al-Khamis- Mfungo tatu /1443 baada ya Hijrah sawa na 7-Jul-2022M
Tembelea Chanel yetu: ☟
https://t.me/Majmuutulaabifiqhishafii
Group la WhatsApp:☟
https://chat.whatsapp.com/LCmiCMbfYC2BHFpca0NFy2
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Jiunge telegram ya faida mchanganyiko :