HUKUMU YA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA WAPENDANAO (VALENTINE DAY)

الشيخ العلامة محمد ابن صالح العثيمين – رحمه الله –

Mwanachuoni mkubwa Muhammad bin Swaalih Al-uthaimin – Allah amrahamu –

السُّؤَالُ:

Swali: 🔊

انتشر في الآونة الأخيرة الاحتفال بعيد الحب خاصة بين الطالبات وهو عيد من أعياد النصارى،

Kumeenea katika kipindi hiki cha mwisho kusherehekea sikukuu ya kupendana haswa baina ya wanafunzi wa kike nayo ni sikukuu katika sikukuu za Manaswara (Wakristo),

ويكون الزي كاملا باللون الأحمر،
الملبس والحذاء، ويتبادلن الزهور الحمراء،

(Usherehekeaji wake) unakua kwa (kuvaa) pambo kamili jekundu, nguo, viatu, na (huwa) wanabadilishana (kwa kupeana) maua mekundu,

نأمل من فضيلتكم بيان حكم الاحتفال بمثل هذا العيد،

Tunataraji kutoka kwenu wabora kubainisha hukumu ya kusherehekea mfano wa sikukuu hizi,

وما توجيهكم للمسلمين في مثل هذه الأمور والله يحفظكم ويرعاكم؟

Na ni upi muongozo wenu kwa waislamu katika mfano wa mambo haya na Allah akuhifadhini na akuchungeni?

الجَـوَاب:

Jawabu: 📚

الاحتفال بعيد الحب لا يجوز لوجوه:

Kusherehekea sikukuu ya wapendanao haifai kwa sababu (nyingi):

١ – الأول:

1 – Ya kwanza :

أنه عيد بدعي لا أساس له في الشريعة.

Kwamba hiyo ni sikukuu ya kibidaa/kizushi haina misingi katika sheria.

٢ – الثاني:

2 -Ya pili:

أنه يدعو إلى العشق والغرام.

Kwamba hiyo (sikukuu) hulingania katika ashqi, na mapenzi ya kupindukia.

٣ – الثالث:

3 – Ya tatu:

أنه يدعو إلى اشتغال القلب بمثل هذه الأمور التافهة المخالفة لهدي السلف الصالح رضي الله عنهم.

Kwamba hiyo (sikukuu) hulingania katika kuushughulisha moyo kwa mambo haya yasiyo kuwa na maana (dhalili) yanayoenda kinyume na njia ya wema waliopita.

فلا يحل أن يحدث في هذا اليوم شيء من شعائر العيد

Basi (kama ni hivyo) haifai kufanywa katika siku hii (ya velentine day) chochote katika nembo (alama) za sikukuu,

سواء كان في المآكل، أو المشارب، أو الملابس، أو التهادي، أو غير ذلك،

Sawa sawa (iwe) katika vyakula, au vinywaji, au mavazi, au kupeana zawadi au mengineyo yasiyo kuwa hayo,

وعلى المسلم أن يكون عزيزا بدينه وأن لا يكون إمعة يتبع كل ناعق،

Na inawajibika kwa muislamu awe mtukufu (ajivune) kwa dini yake na wala asiwe mwenye kufuata mkumbo (akawa) anamfuata kila mwenye kuitia katika jambo la batili,

أسأل الله تعالى أن يعيذ المسلمين من كل الفتن ما ظهر منها وما بطن، وأن يتولانا بتوليه وتوفيقه.

Namuomba Allah awakinge waislamu kutokana na kila fitna (balaa) zilizodhihiri na zilizojificha na atusimamie kwa usimamizi wake na taufiq yake.

📚 المَصْدَرُ: مجموع فتاوى ابن العثيمين. (١٩٩/١٦)

Maelezo ya mfasiri:

Haifai kwa muislamu kusherehekea sikukuu yeyote ya kikafiri au ya kizushi ,na hutakiwi kufanya chochote ambacho hufanywa katika sikukuu hiyo mfano kuvaa nguo nyekundu tena hata kama haujakusudia kujifananisha na wenye kusherehekea sikukuu hiyo utapata madhambi, maadamu unaijua siku hiyo.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imerushwa mara ya tatu: Mfungo kumi 12, 1443H ≈ Feb 13, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *