HUKUMU YA KUSHIRIKIANA MUME NA MKE KATIKA KICHINJWA CHA UDH’HIYA.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

HUKUMU YA KUSHIRIKIANA MUME NA MKE KATIKA KICHINJWA CHA UDH’HIYAH

سؤال:

Swali:

ما حكم اشتراك الزوجين في ثمن أضحية العيد؟ علما وأنهما مشتركين في مصروف البيت,

Ni ipi hukumu ya kushirikiana mume na mke katika kichinjwa cha udh’hiya ,cha eid?, itambulike kwamba wao wawili wanashirikiana katika matumizi ya nyumbani,

الجواب:

Jawabu:

اذا كانت الزوجة تريد مساعدة الزوج في ثمن الأضحية, فلا بأس في ذلك, بل هو من المعروف،

Pindi atakapokuwa mke anakusudia kumsaidia mume katika thamani ya kichinjwa cha udhuhiya basi hakuna ubaya katika hilo bali hilo ni katika wema,

أمّا إذا كانت تريد أن تضحي عن نفسها, أضحية خاصة, فلا يصح ان تشاركه في الشاة والضأن،

Ama atakapokuwa (mke) anataka kujichinjia udh’hiya mwenyewe (yaani) udh’hiya maalumu, basi haifai kushirikiana na huyo (mume) katika mbuzi na kondoo,

لكن لها أن تشاركه في سبع بقرة أو بدنة,

Lakini (mke) anaruhusiwa kushirikiana na huyo (mume) katika (thamani ya) moja ya saba ya ngo’mbe au ngamia,

فتدفع هي قيمة سبع وهو يدفع قيمة سبع آخر، والله اعلم.

basi atatoa huyo (mwanamke) thamani ya moja ya saba, na yeye (mume) atatoa thamani
ya moja ya saba nyingine.

Na Allah ni mjuzi zaidi

محمد بازمول.

Muhammad Baazamuul

أعيد نشرها في ٢٣ ذي القعدة ١٤٤١هجرية.

[ Imerudiwa kurushwa 23 dhulqaa’dah mwaka 1441 Hijiria ]

المصدر:
www.bamool.net

Maelezo:

Kwa maana haifai mke kushirikiana na mume katika kumiliki kichinjwa cha udh’hiya cha mbuzi/kondoo, ama kumshirikisha mumewe na familia yake katika thawabu hili linafaa kwa maana mke akamiliki kichinjwa na akaishirikisha familia katika thawabu ya udh’hiyah kwa maana akakichinja hicho kichinjwa kwa niaba yake na familia yake akiwemo mumewe

Ama mke akaamua kumchangia mumewe pesa ya kununua mbuzi wa udh’hiya yaani huyu mbuzi atamilikiwa na mume kwa maana atakuwa wake kisha mume atakapochinja ataishirikisha familia yake katika thawabu akiwemo mkewe, hili linaruhisiwa kwa mke.

Ama mbuzi mmoja wa udh’hiya wakashirikiana katika kummiliki zaidi ya watu wawili kama vile mume na mke ,au wawili wowote hili halifai, ama kikiwa kichinjwa ni ngamia au ng’ombe wanaruhusiwa kushirikiana katika kumiliki kichinjwa hicho watu saba kila mmoja akatoa moja ya saba ya thamani yake, mfano mke na mume nao wanaweza wakashirikana katika kumiliki katika hali hii katika kumiliki ngamia au ng’ombe.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Iliandaliwa: Dhul-Hijjah 6-1441H=27-July-2020M ,ikarushwa tena Dhul-Hijjah 2-1442H =12-Jul- 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

  1. Ally MTAWATAWA

    Allah atawapeni kwa elimu mnayo itoa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *