HUKUMU YA KUSHIRIKIANA NA MANASWARA/WAKRISTO KATIKA KATIKA SIKUKUU YA CRISTMAS

للشيخ صالح الفوزان – حفظه الله تعالى

(Jawabu la) Sheikh Swalih Al-fauzan – Allah aliyetukuka amuhifadhi.

السؤال:

مع دخول هذا الشهر الميلادي تبدأ احتفالات النصارى بالكريسمس وأعيادهم، ما حكم مشاركتهم في احتفالاتهم سواء بعملها أو حضورها أو تبادل الهدايا فيها أو التهاني؟

Swali:

Kwa kuingia mwezi huu wa kikristo zinaanza sherehe za Wakristo Christmas na sikukuu zao (nyingine), basi ni ipi hukumu ya kushirikiana nao katika sherehe zao sawa sawa kwa kusherehekea au kuhudhuria au kupeana zawadi katika hizo (sikukuu) au kupongezana?

الجواب:

لا يجوز كل هذا، لا يجوز مشاركتهم و حضورها الله – جلَّ وعلا- قال:

{ وَالَّذِينَ لا يَشْهَدُونَ الزُّورَ }

يعني لا يحضرون أعياد الكفار، لأن حضورهم فيها إقرار لها ورضىً بالمنكر وهذا لا يجوز ،ولا تهنئتهم فيها لا يجوز هذا كله؛

لأنها أعياد مبتدعة حتى في دين النصارى ماهي بمشروعة إنما هم ابتدعوها.

Jawabu:

Hayafai yote haya, haifai kushirikiana nao na kuhudhuria (sherehe) hizo, Allah – aliyeshinda na kutukuka – anasema:

{ Na wale ambao hawahudhurii uzushi }

Maana yake: Hawahudhurii sikukuu za makafiri kwa sababu kuhudhuria kwao katika hizo (sikukuu) na kuzikubali na kuridhia uovu na hili halifai na wala (haifai) kuwapongeza katika hilo na hayafai yote haya;

Kwa sababu hizo ni sikukuu zilizozushwa, hata katika dini ya Manaswara (wenyewe), hazipo hakika si vinginevyo wao wamezizusha.

المصدر:

Maelezo ya mfasiri:

Haifai kushirikiana na Makafiri katika sikukuu zao kwa lolote lile ambalo linahusu sikukuu hizo , na hapo sheikh amenukuu aya katika suratul-furqan ambayo inataja miongoni mwa sifa za waumini ni kutohudhuria sikukuu za Makafiri nayo ni kauli yake Allah :

{ وَٱلَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ ٱلزُّورَ }

{Na wale ambao hawahudhurii uzushi} .

الفرقان ٧٢

Makusudio ya uzushi hapa ni sikukuu za Makafiri na washirikina kama walivyotafsiri wanavyuoni wengi zaidi wa tafsiri.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imerudiwa :Mfungo nane 21, 1443H ≈ Dec 25, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *