Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
” أبراج الحظ يحرم نشرها والنظر فيها وترويجها بين الناس، ولا يجوز تصديقهم، بل هو من شعب الكفر والقدح في التوحيد،
” Ni haramu kuzisambaza nyota za bahati na kutezama ndani yake na kuzitawanya baina ya watu ,na wala haifai kuwasadikisha hao (wanajimu), bali hayo (matendo) ni katika matawi ya ukafiri na ni kuitia dosari tauhid,
والواجب الحذر من ذلك، والتواصي بتركه، والاعتماد على الله سبحانه وتعالى، والتوكل عليه في كل الأمور “.
na linalowajibika ni kuwa na tahadhari na hilo, na kuusiana kuliacha (jambo) hilo , na kumtegemea Allah -utakasifu ni wake na ametukuka- na kutegemea juu yake katika mambo yote “
Chimbuko:
” فتاوى اللجنة الدائمة ” (٢٧/٢٠٣) :
Maelezo ya mtarjumu:
Haifai kuangalia nyota za bahati kama wenyewe wanavyoziita, wala kusambaza kwa wengine sawa sawa iwe kwa njia ya magazeti au redio ,television ,na njia nyinginezo, na yeyote mwenye kufuatilia nyota yake kwa njia yoyote hata gazeti au redio au television au mitandaoni basi ajue kuwa hukumu yake ni sawa na yule aliyeenda kwa huyo mnajimu au mganga wa kishirikina na swala zake hazikubaliwi kwa muda wa siku arobaini kwa maana hapati thawabu kama ilivyothibiti katika hadithi , na kama akiyasadikisha yale aliyoyasoma au kuangalia basi atakuwa ameyakufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad- swala na salamu za Allah zimfikie- kwa maana atakuwa amefanya dhambi kubwa mno, tena huwenda akatoka katika uislamu .
Waganga wa kishirikina ,wapiga ramli,wanajimu wote hawa ni watu ambao wanadai kujua elimu ya ghaibu ambayo hakuna aijuaye isipokua Allah, kama alivyosema Allah -aliyetukuka-:
قُل لَّا يَعْلَمُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الْغَيْبَ إِلَّا اللَّهُ ۚ
Sema “Hakuna ajuaye Ghayb (yaliyojificha) waliyoko mbinguni na ardhini ila Allah.
النمل : ٦٥
Mwisho :
Wale wenye kufuatilia hizi nyota na wakidai kuwa ni nyota za bahati watambue kuwa yote yanayotokea yamekadiriwa na Allah : kukosa ,kupata ,afya ,maradhi, na hata hiyo bahati na mengineyo yote yamekadiriwa na Allah .
Mtarjumu: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 2, 1443H ≈ October 8, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Ktk haya Allah Atuongoze biidhnihii
Ahsant jazaakallahu jgayra
Ahsant jazaakallahu khayra