HUKUMU YA KUTOA MIMBA

السؤال ٢٠٥:

Swali 205: 📁

هل يجوز إسقاط الحمل في أيامه الأولى‏؟‏

Je, inaruhusiwa kutoa mimba katika siku zake za mwanzo?

الجواب:

Jawabu: 📚

إذا كان الغرض من إسقاط الحمل هو كراهية الحمل وعدم إرادته فهذا لا يجوز‏،

Pindi litapokuwa lengo la kutoa mimba ni kuchukia ujauzito na kutoutaka basi hili halifai,

أما إذا كان لضرورة بأن يخشى على حياة الحامل لو بقي،

Ama ikiwa kwa dharura kama vile kukaogopewa uhai wa mjamzito lau (mimba) itabakia,

وكان في طور النطفة أو العلقة،

Na (mimba) ikawa katika hatua ya tone la manii au pande la damu,

فلا بأس بإسقاطه إذا قرر ذلك هيئة طبية موثوقة‏.‏ 

Basi hakuna ubaya kuitoa (mimba) pindi watakapolithibitisha hilo jopo la tiba lenye kuaminiwa.

📚 المنتقى من فتاوى الشيخ الفوزان.

Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi

Vigawanyo vya hukumu ya kutoa mimba:

1- Hali ya kwanza: Inaruhusiwa kutoa mimba isiyofika siku arobaini (40) kukiwa na haja, kama vile akiwa mwanamke anatumia dawa ambayo haikubaliani na mimba, au akiwa mwanamke amejifungua karibuni kiasi ambacho akibaki na ujauzito ni mashaka makubwa kwake.

2 – Hali ya pili: Mimba itakapozidi siku arobaini (40) kabla ya kupuliziwa roho inaruhusiwa kuitoa kwa dharura mfano: Mwanamke aliyepatwa na maradhi ya hatari madaktari wakamwambia kuwa kutokana na elimu yetu ya tiba usipotumia dawa utakufa na ukitumia dawa hiyo lazima mimba itolewe au itoke, muda huu mwanamke huyu ataruhusiwa kutoa mimba kwa dharura hii maadamu bado haijapuliziwa roho, na wala haifai kuitoa kwa haja kama tulivyoeleza katika hali ya kwanza hapo juu.

3 – Hali ya tatu: Ama mimba ikishapuliziwa roho haifai kutolewa kwa hali yoyote hata kama madaktari watasema kuwa isipotolewa mimba mama atafariki kwa sababu kuitoa mimba baada ya kupuliziwa roho ni kuua nafsi ama maneno ya madaktari hayazingatiwi mia kwa mia kwa sababu huwenda wakasema hivyo na mama akaishi, na hii ndiyo kauli sahihi.

Na Allah ndiye mwenye kutakwa msaada. Tunamuomba Allah afya na salama

Tanbih: Maana ya maelezo haya nimeyatoa katika jibu alilojibu Sheikh Suleiman Arruhailiy – Allah amuhifadhi – kuhusu hukumu ya suala hili.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 13, 1443H ≈ Jun 13, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *