Hukumu ya kutumia mikeka /mazuria ya msikiti kwa matumizi yasiyokuwa ya msikiti .

ﻫﻞ ﻳﺠﻮﺯ اﺳﺘﻌﻤﺎﻝ ﺣﺼﺮ اﻟﻤﺴﺠﺪ ﻭﻓﺮاﺷﻪ ﻟﺤﺎﺟﺎﺕ ﻛﺤﺎﺟﺔ اﻟﻌﺮﺱ،

Je inaruhusiwa kutumia mikeka ya msikiti na mazuria yake kwa ajili ya haja (mbalimbali) kama haja ya harusi,

ﻭﻛﻌﺮﺽ ﺷﻲء ﻛﺎﻟﻜﺘﺐ ﻋﻠﻰ اﻟﺸﻤﺲ ﺇﺫا ﻟﻢ ﻳﻜﻦ ﻣﻨﻪ ﺑﺪ ﺃﻡ ﻻ ؟

kama vile kuanika kitu juani kama vile vitabu ikiwa hakuna budi (kufanya hivyo)

(ﻓﺄﺟﺎﺏ) ﺑﻘﻮﻟﻪ:

Akajibu kwa kusema:

ﻻ ﻳﺠﻮﺯ اﺳﺘﻌﻤﺎﻝ ﺣﺼﺮ اﻟﻤﺴﺠﺪ ﻭﻻ ﻓﺮاﺷﻪ ﻓﻲ ﻏﻴﺮ ﻓﺮﺷﻪ ﻣﻄﻠﻘﺎ ﺳﻮاء ﺃﻛﺎﻥ ﻟﺤﺎﺟﺔ ﺃﻡ ﻻ،

Haifai kutumia mikeka ya msikiti wala mazuria yake katika (matumizi) yasiyokuwa ya kuitandika (hapo msikitini)

ﻭاﺳﺘﻌﻤﺎﻟﻬﺎ ﻓﻲ اﻷﻋﺮاﺱ ﻣﻦ ﺃﻗﺒﺢ اﻟﻤﻨﻜﺮاﺕ اﻟﺘﻲ ﻳﺠﺐ ﻋﻠﻰ ﻛﻞ ﺃﺣﺪ ﺇﻧﻜﺎﺭﻫﺎ،

Na kuitumia harusini ni katika maovu mabaya kabisa ambayo inawajibika juu ya kila mmoja kuyapinga ,

ﻭﻗﺪ ﺷﺪﺩ اﻟﻌﻠﻤﺎء اﻟﻨﻜﻴﺮ ﻋﻠﻰ ﻣﻦ ﻳﻔﺮﺷﻬﺎ ﺑﺎﻷﻋﺮاﺱ ﻭاﻷﻓﺮاﺡ، ﻭﻗﺎﻟﻮا:
Na bila shaka wanavyuoni wameweka mkazo wa katazo juu ya yule mwenye kuyatandika katika harusi na sherehe (mbalimbali) na wakasema:

ﻳﺤﺮﻡ ﻓﺮﺷﻬﺎ ﻭﻟﻮ ﻓﻲ ﻣﺴﺠﺪ ﺁﺧﺮ، ﻭاﻟﻠﻪ ﺳﺒﺤﺎﻧﻪ ﻭﺗﻌﺎﻟﻰ ﺃﻋﻠﻢ”.

Ni haramu kuyatandika hata kama itakuwa katika msikiti mwingine , na Allah aliyetukuka ni mjuzi zaidi .

الفتاوى الفقهية الكبرى للعلامة ابن حجر الهيتمي(٣/ ٢٨٨)

Ufafanuzi wa mfasiri:

Haifai kutumia vitu vya msikitini katika matumizi mengine yasiyokuwa ya msikitini , kama vile :

Mikeka na mazuria ya msikitini ni haramu kutumika katika matumizi mengine yasiyokuwa ya kuyatandika msikitini, na pia yatumike katika msikiti husika.

Tarjama: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Chanel yetu ya telegram👇🏼:

https://t.me/Majmuutulaabifiqhishafii

Watsapp 👇🏼:

https://chat.whatsapp.com/LCmiCMbfYC2BHFpca0NFy2

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *