Makala namba: 2
Aina ya pili ya vyakula:
Vyakula ambavyo muuzaji hajui kuwa mnunuzi atavitumia muda gani mchana au usiku?, kama vile mchele, maharage mabichi, viungo mbalimbali kama vile vitu vya masokoni basi vitu hivi si vibaya kuuuza mchana wa Ramadhani na wala mwenye kuuza hana dhambi katika hilo,
Na hata dhana yake yenye nguvu ikimwambia kuwa huyu mnunuzi hakufunga kwa sababu ya ukafiri wake au muislamu muovu, kwa sababu aina hii ya vyakula anaweza kuvitumia muda ule ule wa mchana au usiku au huwenda akaviweka mpaka vikaharibika asivitumie.
Kwa hiyo asili ya kuuza aina hii ya vyakula ni halali, kwa hiyo kila biashara ambayo una shaka kuwa mnunuzi ataitumia kwa njia ya halali au haramu asili inabakia ni halali, pamoja na kuwa ukiacha kuuuza ni bora zaidi katika hali hii.
Mwisho: Sheria ya kiislamu haijatuamrisha kuwachunguza watu ambao ni wanunuaji wa hivi vyakula ambavyo haviliwi muda ule ule, kwa sababu kuwachunguza ni kujitia uzito na Allah anasema:
(يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ)
{ Allah anawatakia wepesi na wala hawatakii uzito }
البقرة/ ١٨٥.
Kwa kifupi vyakula ambavyo hukumu ya ujumla haihukumu kwamba vitaliwa muda au hakuna sifa ya aghlabu inayoonesha kuwa huliwa muda ule ule hakuna uharamu wa kuuza, ama vile vinavyoliwa muda ule ule, au kufungua migahawa n.k, haya hayafai.
NASAHA ZETU:
Wauza migahawa, mihogo ya kukaanga, maandazi, chapati, ice cream na mfano wa vyakula vinavyoliwa muda huo huo yaani mnunuzi anayenunua unajua kuwa atakula muda ule ule, wanatakiwa waache biashara hizi na wauze biashara ya vitu ambavyo havijulikani kuwa vitaliwa kwa muda ule ule au baadae kama: Mchele, unga, tambi, mihogo mibichi.
Tanbihi: Vyakula hivi ambayo hakuna alama inayoonesha kuwa vitaliwa muda ule ule ni halali kuuza, kwa sababu asili ni halali ila kwa dalili kama vile vyakula tulivyofitaja katika Makala namba: 1
Ama ukijua kwa yakini kuwa anaenda kupika na kula sasa hivi usimuuzie na pia sheria haikukuambia umchunguze.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 15, 1443H ≈ Mar 18, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•