HUKUMU YA KUVAA WIGI /NYWELE ZA BANDIA

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

HUKUMU YA KUVAA WIGI /NYWELE ZA BANDIA .

السؤال (٢٤١)
Swali (241)

سئل العلامة الفوزان -حفظه الله-

Aliulizwa mwanachuoni mkubwa Al-fauzan- Allah amuhifadhi-

ما حكم لبس الباروكة للرجال والنساء وأيضًا ما حكم التمثيل‏؟‏ بالنسبة للرجال وأيضًا للنساء‏؟‏

Ni ipi hukumu ya kuvaa wigi kwa wanamume na wanawake ,na pia hukumu ya kuigiza kwa upande wa wanamume na pia wanawake ?

الجواب
Jawabu:

لا يجوز لبس الباروكة للرجال والنساء أيضًا، أما النساء لأن فيه غشًا وتدليسًا حيث أن الرائي لها يظن أن هذا من خلقتها ومن شعرها الأصلي وهو ليس كذلك وفي هذا تلبيس وتغرير ربما بزوجها أو بمن يريد خطبتها‏.‏

Haifai kuvaa wigi kwa wanamume na wanawake pia ,ama wanawake kwa sababu ndani yake kuna hadaa na udanganyifu kwa upande ambao yule anayemuona huyo (mwanamke) hudhania kuwa haya ni maumbile yake na ni katika nywele zake za asili , na hali ya kuwa si hivyo na katika hili kuna kuchanganya na kuhadaa huwenda (akamhadaa) mumewe au yule anayetaka kumchumbia .

أما الرجل فلا يجوز له ذلك بحال من الأحوال قد يجوز للمرأة مثلاً إذا كانت – ليس لها شعر أصلاً كأن لم ينبت لها شعر أن تلبس الباروكة لأنها أصبحت مضطرّة لذلك ومحتاجة لذلك

ama mwanamume haifai kwake (kufanya) hivyo kwa yoyote ,huwenda likaruhusiwa (hilo) kwa mwanamke mfano akiwa hana nywele kabisa kama akiwa hajaota nywele (muda huo ataruhusiwa) kuvaa wigi kwa sababu amekuwa ni mwenye kudharurika kwa hilo na mwenye haja na hilo ,

أما الرجل فإنه لا يجوز أن يلبس الباروكة بحال ولا سيما إذا كان ذلك لأجل التمثيل

ama mwanamume bila shaka yeye haifai kuvaa wigi hata kidogo haswa ukiwa (huo uvaaji) ni kwa ajili ya kuigiza

فإنه في لبسه لهذا الشعر يظهر بصورة غير صورته الحقيقية وربما تكون صورة فيها تشبّه بالنساء أو تشبّه بالكفار أو غير ذلك‏.‏
bila shaka yeye katika kuvaa kwake hivi nywele (za bandia) atadhihiri katika muonekano usiokuwa wa kweli na huwenda ukawa muonekano ndani yake kuna kujifananisha na wanawake au kijifananisha na makafiri na yasiyokuwa hayo (katika maovu)

__المنتقى من الشيخ الفوزان

Maelezo ya muandaaji :

Haifai kwa mwanamke kuvaa nywele za bandia (wigi) ,kwa sababu hizo alizozitaja sheikh -Allah amuhifadhi- ,ama kwa mwanamume kunaongezeka uharamu wa kujifananisha na wanawake, ama hukumu ya kuigiza /kufanya kazi ya maigizo ,kundi kubwa la wanachuoni limetoa hukumu kuwa ni haramu na ndani yake kuna madhara mengi ,na miongoni mwa wale waliosema kuwa ni haramu ni sheikh ibn Baz – Allah amrahamu- pale alipoulizwa kuhusu maigizo na akajibu hivi :

“أنا لا أنصح بممارسة التمثيل، وإنما على العلماء أن يبينوا للناس أحكام الله ورسوله، أما أن يتقمص المرء شخصية فلان، واسم فلان، فيقول: أنا عمر، أو أنا عثمان.. أو نحو ذلك، فهذا كذب لا يجوز فعله”

” Mimi sitoi nasaha za kufanya maigizo ,na hakika si vinginevyo ni juu ya wanavyuoni wawabainishie watu hukumu za Allah na Mtume wake ama mtu kujivesha utu wa (mtu) fulani ,na jina la fulani ,(mfano) akasema : Mimi Omar au mimi Uthman.. au mfano wa (watu ) hao ,huu ni uwongo haifai kufanywa.

فتاوى الشيخ ابن باز – رحمه الله – (٥/ ٢٧١-٢٧٢)

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Shawwal 28, 1442H ≈ Jun 9, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *