Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
✍🏻قال الشيخ ابن عثيمين -رحمه الله-:
Amesema sheikh ibn ‘Uthaimin- Allah amrahamu-:
“الرموش الصناعية لا تجوز؛ لأنها تشبه الوصل أي وصل شعر الرأس، وقد لعن النبي -صلى الله عليه وسلم- الواصلة والمستوصلة،
Kope za bandia hazifai kwa sababu zinafanana na kuunganisha, nakusudia kuunganisha nywele za kichwa ,na bila shaka Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- amemlaani anayeunganisha (nywele) na anayeunganishwa,
وهذه الرموش إذا كانت مما أتصوره الآن أن يوضع خيوط سوداء كالشعر على الرموش حتى تبدو وكأنها كثيرة تتجمل بها العين فإذا كان هكذا فهي من الوصل الذي لعن النبي -صلى الله عليه وسلم- فاعلته في رأسها،
na hizi kope zikiwa ni katika zile ambazo ninazozifikiria sasa hivi (ambazo) :
Ni kuweka nyuzi nyeusi kama vile nywele juu ya kope (za asili) ili zidhihiri kama vile ni nyingi (ili) jicho lijipambe (lipendeze) ,ikiwa ni hivi basi huko ni katika kuunganisha (nywele) ambako Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- amemlaani mwenye kufanya hivyo kichwani mwake ,
أما إذا كانت الرموش بمعنى تلوين الشعر شعر الأجفان فإنه ليس بحرام. نعم”.
ama kama ikiwa (kuweka) kope kwa maana :Kuzipaka rangi kope basi hilo si haramu .
Ndio (inarahusiwa) .
Chimbuko:
http://binothaimeen.net/content/12137
Maelezo ya mtarjumu:
Sheikh -Allah amrahamu- amesema kuwa haifai kwa mwanamke kuweka kope za bandia kwa sababu kitendo hicho ni sawa na kuunganisha nywele kitendo ambacho Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- amemlaani muunganishaji na muunganishwa ,na akasema kuwa hakuna ubaya wa mwanamke kuzipaka/ kuzibadilisha rangi kope zake za asili ,lakini sheikh hapa anakusudia pia ataruhusiwa kufanya hivyo ikiwa hakutakuwa na madhara katika kufanya hivyo kama vile kutoka vidonda au kupukutika kope n.k, kwa maana kikiwa hicho anachotumia kuzipaka rangi kope kina madhara basi haitofaa, kwa sababu Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- anasema:
“لَا ضَرَرَ وَ لَا ضِرَارَ “
Hakuna kudhuru na wala kurudisha madhara .
Na vile vile mwanamke pindi anapozipamba hizo kope haruhusiwi kudhihiri mbele ya wanaume wanaoruhusiwa kumuoa .
Pia ikiwa hiyo rangi aliyoweka katika kope inazuia kuingia maji katika hizo kope basi anawajibika kuitoa kabla ya kutawadha ili udhu wake uwe sahihi.
Mtarjumu: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Swafar/Mfungo tano 29, 1443H ≈ Oct 6, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•