HUKUMU YA KUZURU MAKABURI SIKU YA EID

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

جاء في فتوى اللجنة الدائمة،
لم يثبت عن النبي- صلى لله عليه وسلم:
أنه كان بخص يوم الجمعة أو يوم العيد بزيارة القبور،
بل كان يزورها دون تحديد يوم،
والخير كل الخير في الاقتداء به.

Yamekuja (maneno) katika fatwa ya kamati ya kudumu :

” Haikuthibiti kutoka kwa Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

kwamba alikuwa akiihusisha siku ya ijumaa au siku ya eid kwa kutembelea (kuzuru) makaburi!

bali alikuwa akiyazuru (makaburi) bila ya kupanga siku maalumu,

na kheri (yaani) kheri zote zipo katika kumfuata yeye (Mtume – swala na salamu za Allah ziwe juu yake”.

📚 فتاوى اللجنة الدائنة – المجموعة الأولى (٩/٦٢-٦٣)

[ Fatawaa ya kamati ya kudumu-mkusanyiko wa kwanza (9/62-63).

Maelezo ya mfasiri:

Ada hii ya kutembelea makaburi siku ya eid hakuifanya Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- kama walivyoeleza masheikh ,na pia haikuwepo kwa wema waliopita ,kama alivyoeleza sheikh Abdul-Qaadir Al-junaid- Allah amuhifadhi- pale aliposema:

📌 تخصيص القبور بالزيارة بعد صلاة العيد.

KUYAHUSISHIA MAKABURI ZIARA BAADA YA SWALA YA EID .

إنَّ طوائف كثيرة جدًا مِن النَّاس قد جعلوا العيد موسمًا لزيارة المقابر والجلوس فيها والتَّجمع عندها، وقراءة الفواتح لأهلها،

Bila shaka makundi wengi mno ya watu waimefanya sikukuu ni msimu wa kuzuru makaburi na kuketi katika hayo (makaburi) na kujikusanya mbele yake na kuwasomea al-fatihah watu wake (maiti) ,

فمَا إنْ ينتهوا مِن صلاة العيد إلا وتوجهوا إليها.

ولا يُعرف هذا الفعل عن سَلف الأمَّة الصالح.

wanapomaliza swala ya eid tu huelekea huko (makaburini) .

Na wala hili tendo halijulikani kutoka kwa wema waliopita wa uma huu .

فما جعلها موسمًا للزِّيارة في العيد، ولا خصَّصها بالزِّيارة فيه رسولُ الله صلى الله عليه وسلم، ولا صحابته ــ رضي الله عنهم ــ،

basi Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- hakuifanya (sikukuu) kuwa msimu wa kuzuru makaburi- na hakuihusisha ziyara ndani ya hiyo (sikukuu) ,na wala maswahaba wake -Allah awaridhie-

ولا مَن بعدهم، ولا أئمة المذاهب الأربعة.

na wala wale waliokuja baada yao na wala maimamu wa madhehebu manne .

وإنْ لم نَقتَد بهؤلاء الأكابر الأجلاء فبِمَن؟

na kama haukuwafuata hawa wakubwa watukufu basi utamfuata nani ?

وأكثر الناس لا يعلمون أنَّ هذه عادة شيعية رافضية، أخذتها عنهم الصوفيه، ونشروها بين أهل السُّنة وبلادهم.

na watu wengi hawajui kuwa hii ni ada ya Mashia wakaichukua kutoka kwao watu wa twariqah na wakaisambaza baina ya watu wa suna na (katika) miji yao .

✏️ وكتبه:
عبد القادر الجنيد.

Ameyaandika: Abdul-Qaadir Al-junaid.

Na pia huku kwetu Tanzania katika mwezi huu wa Mfungo tatu wengi katika watu wanauhusisha na kwenda kusafisha makaburi, na wengine wanapofika huko huingia katika ushirikina wa kutambika /kuwaomba maiti.

Hatukatai kuwa makaburi ya waislamu yanatakiwa yatunzwe bila ya kuchupa mipaka ,lakini kuweka siku siku au mwezi maalumu kwa ajili ya jambo hili huu ni uzushi ,ama kwenda kutambika yaani kuwaomba maiti huu ni ushirikina mkubwa unaomtoa mtu katika uislamu .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 10, 1442H ≈ Jul 20, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *