HUKUMU YA MKE KUNENGUA /KUCHEZA MBELE YA MUMEWE

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

HUKUMU YA MKE KUNENGUA (KUCHEZA) MBELE YA MUMEWE.

الشيخ محمد بن صالح العثيمين – رحمه الله

Sheikh Muhammad bin Swaleh Al-uthaimin – Allah amrahamu

الســـــــؤال :

Swali: 🔊

إذا طلب الزوج من زوجته أن ترقص له، فهل يجب أن تطيعه ؟

Mume atakapomtaka mke wake amnengulie (acheze),

Je, inawajibika (mke) kumtii huyo (mume wake)?

الجــــــــواب:

Jawabu: 📚

أما رقص المرأة أمام زوجها،وليس عندهما أحد ، فلا بأس،

Ama kunengua (kucheza) mwanamke mbele ya mume wake,
na kukawa hakuna mbele yao (mtu) yeyote,
(hilo) halina ubaya,

لأن ذلك،
ربما يكون أدعى لرغبة الزوج فيها،

Kwa sababu jambo hilo,
huwenda likapelekea (kuzidisha) zaidi mapenzi ya mume kwa huyo (mke wake),

وكل ما كان أدعى لرغبة الزوج فيها، فإنه مطلوب،

Na kila lile ambalo linapelekea (kuzidisha) mapenzi ya mume kwa huyo (mkewe),
basi bila shaka (jambo) hilo linatakiwa (kufanywa),

ما لم يكن محرَّماً بعينه، ولهذا,

Madamu halija haramishwa kwa dhati yake,

na kwa sababu hii,

يسن للمرأة أن تتجمل لزوجها، كما يسن للزوج أيضا أن يتجمل لزوجته

inasuniwa kwa mwanamke kujipamba (kujipodoa) kwa ajili ya mume wake,
kama inavyo suniwa pia kwa mume vilevile kujipamba kwa ajili ya mke wake,

كما تتجمل له،

Kama anavyo jipamba (mke) kwa ajili yake (mume),

📚المصدر: اللقاء الشهري (١٢ / السؤال رقم ٩)

Maelezo kutoka kwa mpitiaji – Allah amuhifadhi

Kama alivyoeleza Sheikh kwamba mwanamke anaruhusiwa kunengua (kucheza) mbele ya mume wake, lakini inatakiwa bali inawajibika alifanye hili wakiwa wao wawili tu kusiwepo mwingine yeyote hata watoto wao wasiwepo,

Na pia asiwe anatizama picha na waimbaji mbali mbali ili ajifundishe mitindo ya unenguaji (uchezaji), kwa maana asicheze kwa kuwaiga wanenguaji mbalimbali waovu, bali anengue vile anavyojua kwa asili yake,

Na pia kusiwepo na mziki, kwa maana asiweke mziki kisha akawa anacheza hili halifai bali ni haramu.

Pia mwanamke anaruhusiwa kuvaa vinguo vifupi na vya kubana kwa ajili ya mume wake tu kama alivyofutu hivyo Sheikh Al-baaniy -Allah amrahamu-

[ Sikiliza kaseti namba (814) Silsitul-hudaa wannuur ]

Tanbih: Mke haruhusiwi bali ni haramu kumtii mume wake katika jambo ambalo limeharamishwa kwa dhati yake mfano: kuweka mziki na kucheza, kumwingilia kinyume na maumbile, au kumnunulia kilevi na mambo mengine yenye kuvuka mipaka ya Allah!

Ama jambo la mke kujipamba na kuleta madoido mbele ya mume wake hili linaruhusiwa bali ni sunnah kwa mwanamke kulifanya mbele ya mume wake, limeharamishwa kwa asiyekuwa mumewe kwa vile ni njia ya kufanyika machafu.

Mpitiaji: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Ilindaliwa: January 30,2019M , Toleo la pili: Mfungo sita 29, 1443H ≈ November 4, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

  1. Abuu Mujtaba Mwinyiwiwa

    Baaraka llahu fiykum

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *