Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
HUKUMU YA (MKE) KUNYANYUA SAUTI JUU YA MUMEWE!
سئل الشيخ ابن عثيمين – رحمه الله -:
Aliulizwa Sheikh Ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu –
ما حكم الزوجة التي ترفع صوتها على الزوج في أمور حياتهم الزوجية ؟
Ni ipi hukumu ya mke anayepandisha sauti yake juu ya mumewe katika (maongezi) ya mambo ya maisha yao ya ndoa ?
فأجاب – رحمه الله تعالى:
نقول لهذه الزوجة إن رفع صوتها على زوجها من سوء الأدب ،
Basi (Sheikh) – Allah aliyetukuka amrahamu – akajibu:
Tunamwambia huyu mke bila shaka kunyanyua sauti yake juu ya mumewe ni katika adabu mbaya,
وذلك لأن الزوج هو القوام عليها، وهو الراعي لها،
Na hilo ni kwa sababu mume huyo ni msimamizi juu yake,
na huyo (mumewe) ndiye mchungaji wake,
فينبغي أن تحترمه وأن تخاطبه بالأدب، لأن ذلك أحرى أن يؤدم بينكما
Basi inatakikana amuheshimu na amzungumzishe kwa adabu,
kwa sababu hilo ni bora zaidi (linalopelekea) mkusanyike baina yenu (mke na mume) kwa upendo,
وأن تبقى الألفة بينهما.
كما أن الزوج أيضًا يعاشرها كذلك .
na kubakia mazoea baina ya wawili hao (wanandoa) .
kama inavyotakiwa mume pia aishi nae huyo (mkewe) hivyo hivyo (kwa wema),
فالعشرة متبادلة،
Basi kuishi kwa wema (ni jambo) la kubadilishana (la pande mbili),
قال الله – تبارك وتعالى:
Amesema Allah – aliyezidi kheri na aliyetukuka:
{ وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ فَإِنْ كَرِهْتُمُوهُنَّ فَعَسَى أَنْ تَكْرَهُوا شَيْئاً وَيَجْعَلَ اللَّهُ فِيهِ خَيْراً كَثِيراً }.
{ Na kaeni nao kwa wema, na kama mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Allah akajaalia kheri nyingi ndani yake }
فنصيحتي لهذه الزوجة؛ أن تتقي الله عزوجل في نفسها وزوجها .
Basi nasaha zangu kwa huyu mke;
Amche Allah – aliyeshinda na kutukuka – katika nafsi yake na mumewe,
وأن لا ترفع صوتها عليه،لا سيما إذا كان هو يخاطبها بهدوء وخفض الصوت .
Na wala asinyanyue sauti yake juu ya (mumewe),
na haswa pindi atakapokuwa huyo (mumewe) anamsemesha kwa utulivu na kwa kushusha sauti.
📚 فتاوى نور على الدرب (٢/١٩) – بترقيم الشاملة
Maelezo kutoka kwa Mfasiri – Allah amuhifadhi
Tunawausia wanawake kushusha sauti zao mbele ya waume zao, tizama tabia za wanawake wema walivyokuwa kwa waume zao;
قالت امرأة سعيد بن المسيب – رحمه الله –
Alisema mke wa Sa’iid bin Al-musayyib – Allah amrahamu –
” ما كنا نكلم أزواجنا إلا كما تكلمون أمراءكم “
“ Tulikuwa hatuwasemeshi waume zetu ila kama mnavyowasemesha viongozi wenu ”
📚 حلية الأولياء (١٦٨/٥)
Unapoongea na kiongozi ni lazima uongee nae kwa adabu na heshima tena tumekatazwa kuwasema viongozi kwa uwazi, basi na mume ni hivi hivi anatakiwa mke azungumze nae kwa adabu na taadhima kama walivyokuwa wanawake wa wema waliopita walikuwa wakiwaheshimu waume zao na kuwaogopa uwoga wa heshima. Tunamuomba Allah atupe hifadhi katika ndoa zetu
Muandishi: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la kwanza: January 9,2020M, toleo la pili: Mfungo sita 12, 1443H ≈ October 18, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Masha Allah Allah amuhifadhi shekh wetu tuendelee kupata faida zaidi InshaAllah