HUKUMU YA MSOMAJI RUQYA WA KIUME KUMGUSA MWANAMKE WAKATI ANAPOMSOMEA RUQYA .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

HUKUMU YA MSOMAJI RUQYA WA KIUME KUMGUSA MWANAMKE WAKATI ANAPOMSOMEA RUQYA.

•السؤال:

Swali:

مس جسد المرأة يدها أو جبهتها أو رقبتها مباشرة من غير حائل، بحجة الضغط والتضييق على ما فيها من الجان،

Kuugusa mwili wa mwanamke (au) mkono wake au paji lake la uso au shingo yake moja kwa moja bila ya kizuizi Kwa hoja ya kumkandamiza na kumbana jini aliyopo ndani ya (mwili) wake,

خاصة أن مثل هذا اللمس يحصل من الأطباء في المستشفيات، وما هي الضوابط في ذلك ؟

na haswa mfano wa huku kugusa (mwili) hutokea kwa madaktari mahospitalini , na vipi vidhibiti vya (kuruhusiwa) hilo ?

✍🏻الجواب:
Jawabu:

لا يجوز للراقي مس شيء من بدن المرأة التي يرقيها؛ لما في ذلك من الفتنة، وإنما يقرأ عليها بدون مس ،

Haifai Kwa msomaji ruqya kugusa chochote katika mwili wa mwanamke ambaye anamsomea ruqya kwa sababu ya fitna iliyopo katika hilo, na hakika si vinginevyo amsomee bila ya kumgusa,

وهناك فرق بين عمل الراقي وعمل الطبيب؛ لأن الطبيب قد لا يمكنه العلاج إلا بمس الموضع الذي يريد أن يعالجه،

na kuna tofauti baina ya kazi ya msomaji ruqya na kazi ya daktari, kwa sababu daktari huwenda asiweze kutibu ila kwa kugusa sehemu ambayo anahitaji kuitibu,

بخلاف الراقي فإن عمله وهو القراءة والنفث لا يتوقف على اللمس”.

kinyume na msomaji ruqyah ,kwani kazi yake ni kusoma na kupulizia na wala (kazi yake) haisimamii juu ya kugusa (kiungo ktk mwili) .

📚فتاوى اللجنة الدائمة – المجموعة الثانية.

Maelezo ya mtarjumu:

Haya ni miongoni mwa makosa wanayoyafanya wasomaji ruqya kwa sababu ya kutorejea kwao kwa wanavyuoni, kwa hiyo miongoni makosa wanayoyafanya wasomaji wa ruqya ni kuwagusa, na kuwashika wanawake katika miili yao.

Sheria imeharamisha kumgusa mwanamke wa kando yaani mwanamke unayeruhusiwa kumuoa kama alivyosema Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie-:

لَأنْ يُطعَنَ في رأسِ رجلٍ بِمِخْيَطٍ من حديدٍ خيرٌ من أن يمَسَّ امرأةً لا تَحِلُّ له

Mmoja wenu kuchomwa kichwani kwake kwa sindano kubwa ya chuma ni bora kuliko kumgusa mwanamke asiyekuwa halali kwake .

السلسلة الصحيحة .

Tanbih:

Daktari wa kiume ataruhusiwa kumshika kiungo mgonjwa wa kike kukiwa kuna dharura au haja ya hilo kama vile ikiwa hakuna daktari wa kike mjuzi wa maradhi hayo, na huyo daktari wa kiume atamshika mgonjwa wa kike kadri ya haja kwa maana pale anapomuhitajia kushika tu, tena haruhusiwi kujitenga na mgonjwa wa kike ila akiwa na mumewe au mahram wake kama kaka yake n.k , na vile vile daktari wa kike haruhusiwi kujitenga na mgonjwa wa kiume peke yake , kama chumbani kukiwa na haja au dharura ya kumtibia .

Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshaafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Ramadhani 1, 1442H ≈ April 12, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *