https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
السؤال (٢٤٧)
Swali (247)
سئل العلامة الفوزان -حفظه الله-
Aliulizwa mwanachuoni mkubwa Al-fauzan -Allah amuhifadhi .
ما حكم الشرع في تزين المرأة؟
Hipi hukumu ya kisheria katika mwanamke kujipamba ?
الجواب
Jawabu :
تزين المرأة بما أباح الله لها من الثياب والحلي والكحل والأصباغ والخضاب وقص الأظافر ونتف الإبط والعانة لا بأس به
Mwanamke kujipamba kwa yale (mapambo) aliyomhalalishia Allah katika nguo na mapambo ,kupaka wanja,kupaka rangi nywele au kuzibadilisha (kama kwa hinnah n.k) ,na kukata kucha na kunyofoa (nywele za) makwapa na (kunyoa) nywele za sehemu za siri ,hakuna ubaya (wa) hayo.
بل هو سنة بشرط أن لا تظهر ثيابها وحليها أمام الرجال الذين هم ليسوا من محارمها.
bali (kuyafanya) hayo ni suna ,(kwa hiyo ajipambe) kwa sharti kusidhihiri nguo zake na mapambo yake mbele ya wanamume ambao si katika wale ambao ni haramu kumuoa yeye milele .
أما تزينها بما حرم الله من النمص وهو أخذ شعر الحاجبين وتفليج الأسنان ووشرهن فهذا لا يجوز كله لأن ذلك تغيير لخلق الله تعالى وقد لعن الرسول صلى الله عليه وسلم من فعلته
ama kujipamba kwake kwa yale (mapambo) aliyoyaharamisha Allah kama vile kutoa nyusi (za macho) mawili ,na kuyatanua /kuyaweka mianya meno na kuyachonga , haya yote hayafai kwa sababu (kufanya) hivyo ni kubadilisha maumbile (aliyoyaumba) Allah -aliyetukuka- ,na bila shaka Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- amemlaani yule aliyeyafanya hayo .
المنتقى من فتاوى الشيخ الفوزان
Maelezo ya muandaaji :
Mwanamke hakatazwi kujipamba kwa mapambo ya halali ,bali anatakiwa ajipambe anapokuwa nyumbani na mumewe , bali kuna mapambo ambayo haitakikani kwa muislamu wa kike au wakiume kuyaacha ambayo ni mwenendo wa manabii kama vile : Kukata kucha ,kunyofoa nywele za makwapa kwa mwenye kuweza na kama mtu hawezi basi atatumia nyembe ,lakini kunyofoa ni bora zaidi kwa sababu ni sababu ya kuchelewa kuota tena, na kunyoa nywele za sehemu za siri , kupunguza masharubu kwa wanamume , na haitakikani kuacha kufanya usafi wa sehemu hizi za mwili zaidi ya siku arobaini .
Ama kujipamba kwa kunyofoa nyusi au kuzipunguza zikawa kama mwezi muandamo ,kutanua meno ,n.k kufanya hivi ni haramu ,na ni katika sababu za kupata laana.
Tanbih: Mwanamke anapoziremba nywele zake kwa kuziweka rangi kama hina n.k , anatakiwa asitumie rangi au mtindo ambao ndani yake kuna kujifananisha na wanawake wakikafiri au waovu mbalimbali ,na pia kwa sharti kile atachotumia kisiwe na madhara .
Mwanamke anapojipamba haruhusiwi yaani ni haramu kwake kudhihiri na mapambo yake kwa wale wanamume wanaoruhusiwa kumuoa.
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 28, 1442H ≈ Jun 9, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•