حڪم قـول المـرأة للـرجـل الأجنـبيـﮯ: أحبڪ فيـﮯ اللّـہ
Hukumu ya mwanamke kumwambia mwanaume wa kando: Nakupenda kwa ajili ya Allah
الشــيخ العـلامــة عــبد الـرزاق بن البـدر – حفظـہ اللـہ تعالـﮯ –
Sheikh mwanachuoni mkubwa Abdul-Rrazzaaq bin Al-badr – Allah amuhifadhi-:
السُّـؤَالُ: هذا يسأل يقول: نسمع في بعض البرامج التِّلفزيونيَّة أنَّ بعضَ النِّساء عندما تسألُ تقول للشَّيخ: إنِّي أُحبُّك في الله
Swali: Huyu (muulizaji) anauliza anasema: Tunasikia katika baadhi ya vipindi vya television kuwa baadhi ya wanawake pindi wanapouliza humwambia Sheikh: Hakika mimi nakupenda kwa ajili ya Allah.
الجَـوَابُ:
هذا لا يصلُح، لا يصلُح أنْ تقول المرأةُ لرجلٍ سواءً كان شيخًا أو غيرَه، لا يصلُح أنْ تقول مِثل هذه الكلمة لرجلٍ إلاَّ إذا كان أخاها أو أباها أو زوجها أو نحو ذلك؛ فلا بأس بذلك
Jawbu:
(Jambo) hili halifai, haifai mwanamke kumwambia mwanaume sawa sawa awe Sheikh au asiyekuwa huyo (Sheikh) haifai (kwa mwanamke) kumwambia mwanaume ila akiwa kaka yake au baba yake au mumewe au mfano wa hao, basi (muda huo) hakuna ubaya wa hilo.
أمَّا الرَّجل الأجنبيِّ فهذا بابُ فتنة فلا يصلُح أنْ تقول له: إنَّني أُحبُّك في الله، وإذا أحبَّتهُ في الله تدعو لهُ بظهرالغيب، وتدعو لعموم المُسلمين بظهر الغيب، وفي ذلك كِفاية، نعم
Ama mwanamke (kumwambia) mwanaume wa kando huu ni mlango wa fitna, basi haifai kwa (mwanamke) kumwambia mwanaume: Hakika mimi nakupenda kwa ajili ya Allah na pindi atakapompenda kwa ajili ya Allah, amuombee dua katika hali ya kuwa mwenyewe hayupo (kwa siri) na awaombee waislamu wote katika hali ya kuwa hawapo (kwa siri) na katika huko (kuomba dua) kunatosha, ndio.
المَـصْــدَر مِـنْ هُنـا:
https://www.ajurry.com/vb/archive/index.php/t-42819.html
Maelezo ya Mfasiri: Haifai mwanamke kumwambia Sheikh kuwa na kupenda kwa ajili ya Allah na kumwambia mwanaume yeyote ambaye anaruhusiwa kumuoa kama vile binamu, kaka ambae ni mtoto wa baba mdogo /mkubwa na kaka wa mama mdogo /mkubwa, mashemeji n.k, Na pia haifai kuamiliana nao muamala wowote ambao ni njia ya kufungua mlango wa fitna na balaa la uzinifu, kama vile kumpigia simu na kuongea kwa sauti nyororo au kumpigia simu bila ya haja n.k.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net Imeandaliwa: Tarehe 25 – Safar – 1442H ≈ 12 – October – 2020M.
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•