Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
HUKUMU YA MWANAMKE KUONGEA NA MUUZAJI .
•سئل الشّيخ الدكتور صالح الفوزان -حفظه اللّٰه-: ما حكم تحدث المرأة مع البائع؟
Aliulizwa sheikh duktur Swaleh Al-fauzan-Allah amuhifadhi- ni ipi hukumu ya mwanamke kuongea na muuzaji ?
✍🏻فأجاب:
Akajibu:
تحدث المرأة مع صاحب المتجر التحدث الذي بقدر الحاجة وليس فيه فتنة لا بأس به،
Mwanamke kuzungumza na mfanya biashara uzungumzaji ambao ni kadri ya haja na (uzungumzaji ambao) hauna fitna ndani yake, hilo halina ubaya .
كانت النساء تكلم الرجال في الحاجات والأمور التي لا فتنة فيها وفي حدود الحاجة.
wanawake walikuwa wakiwasemesha wanaume katika haja (mbali mbali) ,na mambo ambayo hayana fitna ndani yake na kwa kadri ya haja .
◾️ أما إذا كان مصحوبًا بضحك أو بمباسطة أو بصوت فاتن؛ فهذا محرم لا يجوز، لقوله تعالى: ﴿فلا تخضعن بالقول فيطمع الذي في قلبه مرض وقلن قولا معروفاً﴾.
Ama yakiwa (mazungumzo) yameambatana na kicheko au kujilainisha au kwa sauti yenye kufitinisha, hili ni haramu halifai ,kwa kauli yake (Allah) aliyetukuka-:
﴿ فَلَا تَخۡضَعۡنَ بِٱلۡقَوۡلِ فَیَطۡمَعَ ٱلَّذِی فِی قَلۡبِهِۦ
مَرَضࣱ وَقُلۡنَ قَوۡلࣰا مَّعۡرُوفࣰا ﴾
{ msilegeze sauti akatamani mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mazuri }
الأحزاب (٣٢).
والقول المعروف: ما يعرفه الناس وبقدر الحاجة، أما ما زاد عن ذلك؛ بأن كان على طريق الضحك والمباسطة،
Na maneno mazuri : Ni yale wanayoyajua watu na (yawe) kwa kadri ya haja ama yale yanayozidi hayo kama vile kwa njia ya kucheka na kujilainisha ,
أو بصوت فاتن، أو غير ذلك، أو أن تكشف وجهها أمامه، أو تكشف ذراعيها، أو كفيها،
au kwa sauti yenye kufitinisha au (kwa fitna) zisizokuwa hizo,
فهذه كلها محرمات ومنكرات ومن أسباب الفتنة، ومن أسباب الوقوع في الفاحشة”.
basi haya yote ni haramu na maovu na ni katika sababu za fitna na ni katika sababu za kuingia katika machafu .
📚المنتقى من فتاوى الفوزان: (٢٩٢/٣).
Maelezo ya mfasiri :
Hii ndiyo mipaka ya mwanamke katika kuzungumza na wafanya biashara wanaume asikithirishe kuongea nao ila kwa kadri ya haja na bila ya kulegeza sauti na kujilainisha ,na hili ni kama ikitokea huyo mwanamke ameenda dukani mara moja moja ,ama mwanamke kwenda masokoni na kukithirisha mara kwa mara , suala hili sheikh aliulizwa :
ما حكم التردد باستمرار على الأسواق لمعرفة الجديد من السلع ؟
Ni ipi hukumu ya (mwanamke) kuendelea kurudia rudia masokoni kwa ajili ya kujua bidhaa mpya ?
فأجاب :
Akajibu (hivi) :
” مطلوب من المرأة البقاء في بيتها والقيام بأعماله وبتربية أولادها ورعايتهم ؛ فإنها راعية في بيت زوجها ومسؤولية عن رعيتها .
Inatakiwa mwanamke kubakia nyumbani kwake na kuzisimamia kazi zake na kuwalea watoto wake na kuwachunga ,na hakika huyo (mwanamke) ni mchunga katika nyumba ya mumewe na ni mwenye kuulizwa kuhusu uchungaji wake .
قال الله تعالى : ( وَقَرْنَ في بُيُوتِكُنَّ ) أي : الزمن بيوتكن ؛ فلا تخرجن لغير حاجة .
Amesema Allah -aliyetukuka- : {Na kaeni majumbani mwenu}
maana yake : Jilazimisheni na majumba yenu na musitoke bila ya haja .
وقال صلى الله عليه وسلم : ( إن المرأة عورة ، فإذا خرجت استشرفها الشيطان )
Na amesema -swala na salamu za Allah
zimfikie- :
{Bila shaka mwanamke ni uchi na pindi atapotoka Shetani hujiandaa kumpoteza}
وليست معرفة الجديد من السلع حاجة تبرر لها الخروج من بيتها ؛ فالخطر عظيم ، خصوصًا في هذا الزمان الذي كثير فيه الشر “
Na kujua bidhaa mpya si haja inayompa ruhusa ya kutoka nyumbani kwake,na hatari ni kubwa haswa katika zama hizi ambazo zimekithiri shari.
“المنتقى من فتاوى الفوزان” (٦٠/٨).
Kwa hiyo mwanamke ajiepushe kwenda sokoni peke yake ,na kama ikibidi basi aende na mumewe au na kaka yake au yule ambaye ni haramu kumuoa milele ,na hili wanaume na akina baba walijue kwa sababu masokoni ni katika maeneo ambayo imekithiri ndani yake mijibwa mwitu ya kibinadamu yenye kuwamendea wanawake!
Mfasiri: Ismail Seiph Mbonde
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 25, 1442H ≈ August 4, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•
Maa Shaa Allah sino zuri