Hukumu ya mwanamume kukaa siti moja na mwanamke kwenye daladala.

📜السؤال:

ما حكم الجلوس بجانب الرجال في الحافلة؟

Swali:

Ni ipi hukumu ya kukaa pembeni ya wanaume kwenye daladala?

✍🏻قال الشيخ ابن باز -رحمه الله-:

Akasema shekh ibnu Bazi -Allah amrehemu- :

“إذا كان ولابد من الركوب في الحافلات العامة،

Kutakapokuwa hakuna budi kupanda mabasi ya watu wote,(pata sote)

فليكن مركب النساء على حدة وراء الرجال والرجال أمامهم على حدة

Basi sehemu watakayopanda wanawake (na kuketi) iwe peke yao (iwe) nyuma ya wanaume, na wanaume wakae peke yao mbele yao (wanawake)

حتى لا تمس المرأة الرجل وحتى لا يحصل تماس وتقارب يخشى منه الفتنة،

ili mwanamke asimguse mwanamume na ili kusipatikane kugusana na kukaribiana (hali ambazo) zinaogopewa fitna,

ينبغي أن تكون مراكب النساء خلف الرجال والرجال أمامهم يخصص لهؤلاء مراكب ولهؤلاء مراكب.

inatakikana sehemu ya, kupandia wanawake iwe nyuma ya wanaume na wanaume (wawe) mbele yao ,hawa wawekewe sehemu maalumu ya kupanda, na hawa wawekewe sehemu maalumu ya kupanda.

فإذا اضطرت إلى خلاف ذلك فلتحرص على التحجب والتستر والبعد عن مماسة الرجل فيما يسبب الفتنة

na kama utapata dharura ya kuwa kinyume na hivyo, (kuwatenganisha) basi na apupie mwanamke kujihifadhi na kijisitiri na kujiweka mbali na kigusana na mwanamume (na hayo ya kugusana) ni katika yale ambayo yanasababisha fitina

حتى تصل إلى جهتها إذا كانت قريبة لا تعد سفرًا.

(ajichunge) mpaka afike aendako kutakapokuwa ni karibu (ambako) hakuzingatiwi ni safari

أما إن كانت المسافة تعتبر سفرًا فلابد من المحرم؛

ama yatakapokuwa masafa yanazingatiwa kuwa ni safari basi hakuna budi (afuatane) na mahram/mwanamume ambaye ni haramu kumuoa milele.

لقول النبي -ﷺ-: «لا تسافر امرأة إلا مع ذي محرم»،

kwa kauli ya Mtume- swala na salamu za Allah ziwe juu yake- : “Asisafiri mwanamke isipokuwa atakapokuwa na Mahramu”

وعلى كل حالٍ الواجب على النساء والرجال أن يتقوا الله جميعًا وأن يحرصوا على البعد عن أسباب الفتنة”.

Kwa hali yoyote ile lililolawajibu juu ya mwanamke na na mwanamume ni wote wamuogope Allah na wapupie juu ya kujiweka mbali na sababu za fitina.

📚فتاوى نور على الدرب.

Maelezo ya mpitiaji:

Asili zinatakiwa gari za abilia ziwe zimegawanywa sehemu mbili :Sehemu ya mbele ni ya wanamume tu na sehemu ya nyuma ni ya wanawake tu, na kama ikiwa hakuna budi kukaa pamoja basi kila mmoja ajitahidi kujiepusha na kugusana na jinsia nyingine kwa sababu hilo linapelekea fitna ya uzinifu.

Mpitiaji: Ismail

Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane 18, 1443H ≈ Dec 22, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *