HUKUMU YA NDUGU KUINGILIA MAGONVI YA WANANDOA

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

HUKUMU YA NDUGU KUINGILIA
MAGONVI YA WANANDOA

📚قال الشيخ ابن عثيمين رحمه lالله :

Amesema sheikh ibn Uthaimin- Allah amrahamu-:

نحذر الأقارب أن يتدخلوا في شئون الزوجين إلا بطلب من الزوجين. إذا طلب الزوجان أن يتدخل الأقارب من أجل الإصلاح فهذا شيء آخر، والإصلاح خير ،

Tunawatahadharisha ndugu kujiingiza katika mambo ya wanandoa wawili ila wanandoa wakitaka (waingilie),pindi wanandoa wawili wakiwataka wanandugu waingilie kwa ajili ya kupatanisha basi hiki ni kitu kingine (kinachoruhusiwa) , na kupatanisha ni heri,

أما بدون إصلاح فإنه لا يحل للأقارب أن يتدخلوا في شئون الزوجين لا سيما إذا كانوا لا يريدون الإصلاح؛ لأن بعض الأقارب -والعياذ بالله-

ama (kuingilia) pasi na kukusudia kupatanisha bila shaka haifai kwa wanandugu kuingilia katika mambo ya wanandoa wawili na haswa wakiwa (wanandugu) hawataki kusuluhisha kwa sababu baadhi ya wanandugu- Allah atukinge-

يحاولون أن ينتصروا لابنتهم مثلاً، أو إذا كانوا من قبل الزوج يحاولون أن ينتصروا لابنهم،

-mfano -hujaribu kumtetea binti yao au wakiwa (ndugu) upande wa mume hujaribu kumtetea mtoto wao wa kiume,

فتجدهم يؤججون نار الغضب والغيض من الزوجة لزوجها أو من الزوج لزوجته،

basi utawakuta wanawasha moto wa ghadhabu na chuki mke kwa mumewe na mume kwa mkewe ,

ولا شك أن هذا حرام وهو من كبائر الذنوب.

na bila shaka hili (jambo) ni haramu na ni katika madhambi makubwa .

▪️لِقاء الباب المفتوح /للشيخ محمد بن عثيمين رحمه اللّٰه(١٥١)

Maelezo ya mtarjumu:

Bila shaka ni haramu kwa wanandugu kuingilia mizozo baina ya wanandoa bila ya ruhusa yao ,na likiwa lengo la wanandugu ni kuharibu ndoa bila shaka uharamu wake ni mkubwa zaidi.

Tanbih:

Lakini kama wanandugu watagundua kuwa kijana wao ameoa mwanamke ambaye anatabia chafu ,na uchafu wake upo wazi tena huwenda ikawa ndiyo sababu ya huyo kijana kuharibiwa bila shaka ikiwa hali ni hii basi muda huo wanandugu wataruhusiwa kuingilia hiyo ndoa tena hata nguvu itumike ili kumuokoa huyo kijana na mfano wa tukio hili lilitokea kwa kijana mmoja katika kipindi cha sheikh Muqbilu- Allah amrahamu- na ndugu waliingilia wakafanikiwa kumtenganisha na huyo binti, na baada ya hapo kijana akarudi katika hali yake mzuri, na pia upande wa pili yaani kama ndugu watagundua kuwa binti yao ameolewa na mtu mchafu uliokuwa wazi basi wataruhusiwa kuingilia ndoa hiyo ili kumuokoa binti yao .

Kwa hiyo maneno ya sheikh -Allah amrahamu-hayana maana wanandugu wamuache binti yao hata kama wanamuona anaangamia au wamuache kijana wao hata kama wanamuaona anaangamia.

Tanbih:

Ukitaka kujua kisa cha wale ndugu walioingilia ndoa ya kijana wao mpaka wakamtenganisha na yule mwanamke muovu ,hebu soma makala yenye anuani ifuatayo katika tovuti yetu.

ATHARI YA MWANAMKE KATIKA MAISHA YA MUMEWE .Makala namba 5 na namba 6 .

Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 16, 1443H ≈ October 22, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *