عن عبيد بن أمّ كلاب أنّه سمع عُمَر بنُ الخطّاب رضي الله عنه وهو يخطب الناس وهو يقول :
Kutoka kwa ‘Ubaid bin Umm Kilab kwamba yeye alimsikia Umar bin Al-khattwab- Allah amridhie- akiwahutubia watu na hali akisema:
” لا يعجبنّكم مِنَ الرَّجُل طَنْطَنَتُهُ وَ لَكِنَّهُ مَنْ أَدَّى الأَمَانَة ، وَ كَفَّ عَنْ أَعْرَاضِ النَّاس فَهُوَ الرَّجُل “.
” Yasikupendezesheni kutoka kwa mtu maneno yake ,lakini hakika hali ilivyo yule mwenye kutekeleza amana ,na akajizuia na (kuchafua) heshima za watu basi huyo ndiye mwanamume”
📚الزهد لابن المبارك ٢٩٥.
🖇 قال الشيخ عبد الرزاق البدر حفظه الله :
Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq Al-badr -Allah amuhifadhi-:
أي لا تغترّ بتزيين الرّجل حديثه و تزويقه كلامه ،
Maana yake: Usihadaike na mtu kuyapamba mazungumzo yake na kuyaremba maneno yake
فالرجولة حقًّا في أداء الأمانة و عدم إضاعتها ،
Uwanamume wa kweli ni kutekeleza amana na kutoipoteza hiyo (amana)
و في الكفّ عن أعراض النّاس و عدم اقتراضها.
na katika kujizuia (kuchafua) heshima za watu na kutowasengenya .
Maelezo ya mfasiri:
Huyu ndiye mwanamume wa sawa sawa, ambaye amekusanya sifa hizi :
1- Mwenye kutekeleza amana, maana yake : Ni mwenye kutekeleza yote ambayo yanawajibika juu yake.
2- Mwenye kuuzuia ulimi wake na mikono yake na kuwaudhi waislamu na watu wote kwa ujumla kama vile :Kuwasengenya, kuwazushia n.k.
Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa:Mfungo nane 8, 1443H ≈ Dec 12, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•