IBADA INAYOZINGATIWA KWA ALLAH .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net

IBADA INAYOZINGATIWA

💎 قال ابن القيم رحمه الله:

Amesema ibn l-Qayyim- Allah amrahamu-:

▫️قوله تعالى:

{إِنَّا كُنَّا مِنْ قَبْلُ نَدْعُوهُ إِنَّهُ هُوَ الْبَرُّ الرَّحِيمُ}

Kauli yake (Allah) aliyetukuka – (alipowazungumzia watu wa peponi):

{Hakika sisi kabla (ya makazi haya) tulikuwa tukimuomba/ tukimuabudia yeye (Allah): Hakika yeye ni mwingi wa ihsani ,Mwenye huruma.” .

سورة الطور ٢٨ .

فهذا دعاء العبادة، المتضمن للسؤال رغبة ورهبة، والمعنى إنا كنا من قبل نخلص له العبادة، وبهذا استحقوا أن وقاهم عذاب السموم، لا بمجرد السؤال المشترك بين الناجي وغيره ،

Basi hii ni dua ya ibada iliyokusanya maombi (yaliyoambatana) na mapenzi na khofu ,na maana ya (aya hii) : Sisi tulikuwa duniani tukimtakasia ibada ,na kwa ajili hii (watu hawa) wamestahiki kukingwa (na Allah) kutokana na adhabu ya upepo wa Moto , (na hawa) hawakukingwa (kwa yale) maombi tu ambayo (ndani yake) hushirikiana baina ya aliyeokoka (na moto) na mwingine (asiyeokoka)

فإن الله سبحانه يسأله من في السموات ومن في الأرض، والفوز والنجاة إنما هي بإخلاص العبادة لا بمجرد السؤال والطلب.

bila shaka Allah -utakasifu ni wake- wanamuomba wale waliopo mbinguni na wale waliopo ardhini, (lakini) kufaulu na kuokoka, Hakika si vinginevyo (hupatikana) kwa kuitakasa (ibada kwa Allah) si kwa kuomba tu na kuhitaji (kutoka kwa Allah)

📚 بدائع الفوائد( ٣ /٥-٦).

Maelezo :

Watu wapeponi watakuwa wakizungumza na miongoni mwa mazungumzo yao watasema kuwa wao duniani walikuwa wakimuomba Allah yaani wakimuabudia kwa kumtakasia ibada ndiyo maana Allah akawakinga na adhabu ya moto .

Na makusudio ya maombi hapa ni ibada iliyofanywa kwa ajili ya Allah ,na si maombi yaliyoepukana na ikhlaswi kwa sababu wote waliopo mbinguni na ardhini wanamuomba Allah katika hali zao zote kwa maneno au kwa hali zao ,kama vile washirikina wanadai kuwa wao wanamuomba Allah kwa ibada zao za kishirikina,lakini na pia viumbe wote wanamuelekea Allah katika haja zao, mbalimbali lakini maombi yenye faida yaani ibada yenye faida ni ibada inayofanywa kwa ajili ya Allah na kutomshirikisha na chochote na mfanyaji ibada hiyo anaifanya hali ya kuwa ana mapenzi ya thawabu atakazolipwa na Allah ,na ana khofu ya adhabu yake .

Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-Qaadah 4, 1442H ≈ Jun 13, 2021M.

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *