IJUE SIKUKUU YA WATU WA PEPONI NDANI YA PEPO !

قال ابن رجب الحنبلي رحمه الله :

Amesema ibn Rajab Al-Hanbaliy -Allah amrahamu-:

وأما أعياد المؤمنين في الجنة فهي أيام زيارتهم لربهم عز وجل،

Ama sikukuu za waumini peponi, ni zile siku za kumzuru Mola wao mlezi -aliyeshinda na kutukuka- ,

فيزورونه ويكرمهم غاية الكرامة، ويتجلى لهم،

basi watamzuru na atawakirimu ukomo wa kuwakirimu na atajidhihirisha kwao ,

وينظرون إليه، فما أعطاهم شيئاً
هو أحب إليهم من ذلك

na watamtezama,basi hatowapa kitu chochote kinachopendeza zaidi kwao kuliko hicho

وهو الزيادة التي قال الله تعالى فيها:

na hiyo ni ziada ambayo amesema Allah katika (kuizungumzia) hiyo :

﴿ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَى وَزِيَادَةٌ ﴾

Wale waliofanya mema watapata (malipo ya) wema (wao) na zaidi ;

لطائف المعارف : ٢٧٨/١

Maelezo ya mfasiri:

Miongoni mwa itikadi za Ahlu-sunnah ni kuamini kuwa waumini watamuona Allah siku ya kiama uonaji wa kuneemeshwa na kutukuzwa , na pia kuna kiwango cha zaidi ya kumuona Allah nacho ni waumini kumzuru Allah na kumtembelea, katika kila siku inayoafikiana na siku ya Ijumaa hapa duniani ambayo inajulikana kwa jina la siku ya ziada, na makusudio ya kumzuru Allah hapa kama walivyoeleza wanawavyuoni ni kile kitendo cha waumini kumkusudia Allah na kutoka vyumbani mwao na kuelekea kwake kwa ajili ya kumuona na kustarehe kwa karamu yake kwao na takrima .

Tanbih:

Waumini watamuona Allah lakini hawatomdiriki, kwa maana hawatamuona vilivyo kama alivyosema Allah -aliyetukuka-:

لَّا تُدْرِكُهُ ٱلْأَبْصَٰرُ وَهُوَ يُدْرِكُ ٱلْأَبْصَٰرَ ۖ وَهُوَ ٱللَّطِيفُ ٱلْخَبِيرُ

Macho hayatomuona vilivyo ,bali yeye anayaona macho vilivyo .Naye ni mwenye kujua yaliyofichikana na yaliyo dhahiri .

سورة الأنعام 103

Aya hii imeeleza kuwa macho hayatomuona Allah vilivyo lakini yatamuona kwa maana kilichokanushwa hapa ni kule kumuona vilivyo yaani kumzunguka, lakini hakujakanushwa kumuona kama tulivyoona hapo juu kuwa waumini watamuona Allah .

Hitimisho :

Kama kuna sehemu haujafahamu basi wasiliana na mwandishi : 👇🏿

0687297829

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa : Mfungo mosi 6 , 1444H =Apr 15, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
    •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *