JAWABU FUPI KUHUSU MAKALA INAYOSAMBAZWA KUHUSU FUNGA YA SIKU YA ARAFAH .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

JAWABU FUPI KWA MAKALA INAYOSAMBAZWA KUHUSU FUNGA YA SIKU YA ARAFAH .

قال الإمام أبو بكر أحمد بن الحسين البيهقي الشافعي -رحمه الله – (ت ٤٥٨) :

Amesema imamu Abuu Bakr Ahmad bin Al-Husain Al-Baihaqiy Asshaafi’iy – Allah amrahamu – aliyefariki (458 baada ya hijra)

في كتابه السنن الكبرى :

Katika kitabu chake: Assunan l-kubraa : .

  • كتاب الصيام.

بَابُ صَوْمِ يَوْمِ عَرَفَةَ لِغَيْرِ الْحَاجِّ

(hiki ni) kitabu kinachozungumzia hukumu za funga.

(huu ni) mlango wa funga ya Arafa kwa asiyekuwa hujaji.

Maelezo yangu muandaaji:

Mlango huu aliouweka imamu Al-Baihaqiy – Allah amrahamu – upo wazi kabisa katika kujulisha kuwa siku ya Arafah ni sunna kufunga kwa asiyekuwa hujaji, kwa maana mahujaji si sunna kwao kufunga, na ndiyo maana madhehebu ya wanachuoni wengi zaidi kama: Maalikiyah, Mashafii, Mahanaabilah wote hao wanaona kuwa inachukiza kwa mahujaji kufunga siku hii ya Arafa. Hii ina maana asiyekuwa hujaji ni sunna kwake kufunga .

Zifuatazo ni hadithi zinazojulisha hilo :

عن أمِّ الفَضلِ بنت الحارِثِ رَضِيَ اللهُ عنهما:

Kutoka kwa ummu l-Fadhli bint Al-Haarith- Allah awaridhie -:

((أنَّها أرسلَتْ إلى النبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم بقَدَحِ لَبَنٍ، وهو واقفٌ عَشِيَّةَ عَرفةَ، فأخذ بيده فشَرِبَه

“Kuwa yeye alimpelekea Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – kopo lenye maziwa na hali yeye (Mtume) amesimama (viwanja vya Arafa) jioni ya siku ya Arafa, basi (Mtume) – swala na salamu za Allah zimfikie – akalichukua hilo (kopo) kwa mkono wake na akanywa hayo (maziwa) “.

رواه البخاري .

Na dalili ya pili :

عن ابنِ عُمَرَ رَضِيَ اللهُ عنهما

Kutoka kwa ibn Umar – Allah amridhie yeye na baba yake-:

((أنَّه حَجَّ مع النبيِّ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم ثم أبي بكرٍ، ثم عمَرَ، ثم عثمانَ، فلم يَصُمْه أحدٌ منهم

” Kuwa yeye alihiji na Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – kisha (akahiji) na Abuu Bakr, kisha (akahiji) na Umar, kisha (akahiji) na ‘Uthman, basi hakufunga (siku) hiyo (ya Arafah) yeyote (katika hao)” .

رواه الترمذي .

Mchanganuo:

Hizi hadith ni dalili tosha kuwa siku hii ya Arafah Mahujaji walikuwa hawafungi na hekima ya kutofunga wanachuoni wanasema:

Ili wasichoke na kudhoofika wakashindwa kusimama na kuomba dua katika siku hiyo tukufu .

TANBIH:

Siku ya Arafah ni siku ya tarehe tisa (9), ambayo Mahujaji wanasimama katika viwanja vya Arafa. Hatukatai kuwa zamani watu walikuwa wakifunga tarehe tisa (9) kwa mujibu wa muandamo wao kwa sababu hakukuwa na vyombo vya mawasiliano vinavyowajulisha kuwa leo ni tarehe (9) katika nchi ambayo kunatekelezwa ibada ya Hijjah ambayo ni Saudia, kwa hiyo walifunga hivyo, lakini sisi tunajua na tunafahamu kuwa siku fulani Mahujaji wanasimama, bila shaka katika hali hii inapendeza tufuate mahali ambapo tukio la kusimama viwanja vya Arafah linafanyika huko, na wale ambao waliofunga katika tarehe tisa (9) ya nchi zao na hali ya kuwa Mahujaji wamesimama viwanja vya Arafah siku iliyopita, kwa kuwa walikuwa wakifanya hivyo kwa kuamini kuwa hiyo ndiyo siku ambayo Mahujaji wanasimama viwanja vya Arafa kwa sababu ya kutokuwepo mawasiliano basi Allah atawalipa thawabu zao, ama wewe unayefahamu kuwa leo Mahujaji wanasimama katika viwanja vya Arafah, bila shaka unatakiwa ufunge siku hii.

Mwenye kufunga siku ya pili yake, yaani baada ya mahujaji kusimama viwanja vya Arafa, huyo jambo lake tunaliacha kwa Allah.

MWISHO:

Namuomba ndugu yangu aliyeandika makala kuhusu funga ya Arafah na kudai kuwa wenye kusema kuwa funga ya Arafah ina mahusiano na kisimamo cha mahujaji viwanja vya Arafah hao ni Mawahabi !

Je huyu imamu Al-Baihaqiy Asshaafiy -Allah amrahamu- aliyefariki mwaka 458 baada ya hijra naye ni katika hao Mawahabi munaowadai ?

Mwisho namalizia makala yangu kwa kunukuu maneno kutoka katika kitabu chetu kidogo (matni) katika vitabu vyetu vya fiqih ya kishafii nacho ni:- [muqaddimatu l-hadhramiy] pale mtunzi -Allah amrahamu – alipokuwa anaelezea funga za sunna akasema :

ما يتكرَّرُ بتكرر السنين ،وهو صوم يوم عرفة لغير الحاج …

” (Kuna) funga zinazojirudia rudia kwa kujirudia miaka, nazo ni: Funga ya siku ya Arafah kwa asiyekuwa hujaji …” .

Rejea:

المُقَدِّمةُ الحضرمية في فقه السادة الشافعية للعلامة عبد الله بافضل الحضرمي -رحمه الله- .

Nikasema (mwandishi) :

Zingatia kauli yake :

“Funga ya siku ya Arafah kwa asiyekuwa hujaji” .

Pia napenda kuwakumbusha kuwa haya si masuala ya kiitiqadi bali ni masuala ya kifiqih ,ila kuna baadhi ya watu -Allah awaongoze- wanaingiza ushabiki – hata kama kuna uwezekano wa kuungana katika hili ,ndiyo maana mmoja katika mashekhe wa kubwa wa twariqa ya qaadiriyyah yaani ni sufi hapa Tanzania , kwa sasa amefariki yeye alikuwa akiwaambia wafuasi wake kuwa wafunge siku ambayo mahujaji wanasimama viwanja vya Arafah! , sina haja ya kumtaja wenye kufuatilia mambo wanamjua nimetaja hili ili kuweka wazi kuwa hili jambo lipo wazi na wala sikusudii kumtakasa huyu sheikh wa kisufi kwa sababu hakuwa katika njia ya sawa.

والله أعلم .

كتبه : أبو ثرياء إسماعيل بن سيف امبوندي الشَّافِعِيّ .

Imeandika : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Mshafi .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Dhul-hijjah 4, 1442H ≈ Jul 14, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *