Je imamu Shafiy -Allah amrahamu- alikuwa Muwahabi ?

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

سؤال موجه إلى الرافضة ؟

SWALI LINALOELEKEZWA KWA MASHIA:- 🎙

هل الإمام الشافعي كان وهابيا؟!!​

JE, Imamu Ashaafi’iy alikuwa Muwahab ?!!

أخرج الهروي عن يوسف بن يحيى البويطي قال:

{{ سألت الشافعي أأصلي خلف الرافضي ؟

قال : لا تصل خلف الرافضي ولا القدري ولا المرجئ ،قلت: صفهم لنا، قال : من قال : الإيمان قول فهو مىرجئ ، ومن قال: إن أبا بكر وعمر ليسا بإمامين فهو رافضي، ومن جعل المشيئة إلى نفسه فهو قدري }}

Amepokea (maneno haya) Al-harawiy kutoka kwa Yusuph bin Yahya Al-buwaitwiy (kwamba) amesema:

{{ Nilimuuliza Asshaafi’iy -je ni swali nyuma ya Mshia ? akasema (Asshaafi’iy),: Usiswali nyuma ya Mshia wala (nyuma) ya Qadariy na wala nyuma ya Murjia, nikasema (Al-buwaitwiy): Tuelezee sifa zao, akasema (Asshaafi’iy): Yeyote mwenye kusema kuwa imani ni kuzungumza (kwa ulimi tu) basi huyo ni Murjia, na mwenye kusema: Hakika Abuu Bakr na Umar (hawakustahiki) kuwa viongozi wawili basi huyo ni Mshia, na yeyote mwenye kuyajaalia matakwa katika nafsi yake basi huyo ni Qadariy }}

📚 Rejea: ⇊

أورده الذهبي في السير ٣١/١

[ Ameyaleta (maneno haya) Addhahbiy katika Assiyar 10/31 ]

NENO LA MWANDISHI: ✍🏾

Imamu Shafiy- Allah amrahamu- anakusudi hivi: Wasikuswalishe na wasiwe maimamu wako katika swala watu wenye itikadi hizi , na tumeweka kichwa cha habari chenye anuani hiyo kwa sababu mara nyingi Mashia na Masufi /watu wa twariqah na Maibadhi wanapokosolewa na kubainishwa itikadi zao chafu,

huwa wanatabia ya kusema uwongo na kuwahadaa waislamu wasiokuwa na elimu kwa kusema: “Musiwasikilize Hawa ni Mawahabi ni kikundi kilichoanzishwa na Muhammad bin Abdul-Wahhaab ambacho lengo lake ni kuleta faraka na tofauti na chuki baina ya waislamu!.

Lakini cha kushangaza mfano swala la kuwakosoa Mashia na kuitikadi kuwa ni katika vikundi vilivyopotea au vilivyopo nje ya uislamu hili ni jambo maarufu kwa wema waliopita na miongoni mwao ni imamu wetu Asshaafi’iy haya sasa tuambieni Mashia je Asshaafi’iy ni Muwahab?!!

hivi ni vituko jamani kwa sababu imamu Asshaafi’iy amekufa mwaka 204 baada ya hijrah na sheikh Muhammad bin Abdil-Wahhab amekufa mwaka 1206 baada ya hijra!! sijui walikutana wapi?!! amakweli uzushi ni kitu kibaya mno mpaka unamfanya mtu atengeneze uwongo ili watu waichukie haki!!

Na hapa utajua kuwa jina la Uwahabi wanalitumia maadui ili kuupaka matope ule uislamu sahihi kwa kuupachika jina hili la uwahabi .

UFAFANUZI WA MANENO KATIKA MAKALA:- ✍🏾

Arraafidhwiy /mwenye kukataa yaani ni Mshia na wameitwa hivi kwa sababu ya kupinga kwao uongozi wa Abuu Bakr na Umar-Allah awaridhie-.

Al-qadariy ni yule mwenye kupinga Qadar ya Allah wenye kuitikadi kuwa Mwanadamu anajiumbia matendo mwenyewa na Allah hakukadiria chochote na kuna wale waliokuwa wakiitikadi kuwa Allah hujui kitu mpaka kitokee na hawa ni makafiri kabisa.

Murjia ni yule mwenye kuitikadi kuwa imani ni kutamka tu basi yaani ukitamka tamko la tauhid basi wewe ni muumin hata kama moyoni ukapinga na vitendo vyako vikawa viovu!!

━════════ ۞
Mwandishi: Ismail Seiph Mbonde Assha’afiy .
════════
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Toleo la kwanza: Swafar /Mfungo tano 23,1439H sawa na tar.12/11/2017M ,toleo la pili: Muharram /Mfungo nne 9, 1442H ≈ August 18, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *