https://t.me/fawaidussalafiyatz
Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
JE MWENYE HEDHI ANARUHUSIWA KUKETI MSIKITINI ?
السؤال (١٣٠)
Swali (130)
سئل العلامة الفوزان -حفظه الله تعالى – :
Aliulizwa mwanachuoni mkubwa Al-Fauzan- Allah amuhifadhi-:
هل على التي تدخل المسجد الحرام أو النبوي وهي حائض شيء مثل كفارة وهي كانت في وقت ضرورة؟
Je kina wajibika chochote kama kafara juu ya yule ambaye anaingia msikiti mtukufu (wa Makkah) au wa Mtume na hali ya kuwa ana hedhi katika wakati (ambao yeye) ana dharura (ya kuingia) ?
الجواب
Jawabu :
لا يجوز للمرأة الحائض أن تدخل المسجد الحرام ولا غيره من المساجد، لأن النبي صلى الله عليه وسلم نهى الحائض أن تدخل المسجد للجلوس فيه
Haifai kwa mwanamke mwenye hedhi kuingia msikiti mtukufu (wa Makkah) na wala mingineyo katika misikiti, kwa sababu Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- amemkataza mwenye hedhi kuingia msikitini na kuketi ndani yake .
أما مجرد الدخول من غير
جلوس كأن تمر به أو أن تأخذ حاجة منه فليس عليها في ذلك حرج، فمرور الحائض والجنب في المسجد أو دخولهم لأخذ حاجة منه في غير جلوس فيه لا حرج فيه،
ama kuingia tu bila ya kuketi kama vile akapita hapo (msikitini) au akachukua haja (fulani) kutoka humo (msikitini) ,basi hakuna ubaya kwake katika hilo, mwenye mwenye hedhi na mwenye janaba kupita msikitini au kuingia kwao kwa ajili ya kuchukua haja (fulani) kutoka humo (msikitini) bila ya kuketi ndani yake ,hakuna ubaya katika hilo ,
إنما الممنوع هو جلوس من عليه حدث أكبر من حيض أو جنابة في المسجد، وما فعلته إن كنت دخلت في المسجد الحرام أو المسجد النبوي وبقيت فيه وجلست فيه فقد فعلت محرمًا؛ لكن عليك أن تتوبي إلى الله سبحانه وتعالى وتستغفريه ولا تعودي لمثل هذا وليس عليك كفارة في هذا إنما عليك التوبة والاستغفار. والله أعلم.
hakika si vinginevyo linalozuiliwa ni kuketi msikitini kwa yule ambaye ana hadathi kubwa kama hedhi au janaba ,na yale uliyoyafanya (muulizaji) kama ulikuwa umeingia msikitini mtukufu (wa Makkah) au msikiti wa Mtume na ukabakia humo au ukaketi bila shaka umefanya (jambo) la haramu ,lakini ni lazima ulete toba kwa Allah -utakasifu ni wake na ametukuka- na umtake msamaha na wala usirudie (kwa kufanya) kama hili ,na hakuna kafara juu yako katika hili ,hakika si vinginevyo ni juu yako kuleta toba na kuomba msamaha .
Na Allah ni mjuzi zaidi .
المنتقى فتاوى الشيخ الفوزان
Maelezo ya muandaaji:
Haifai na ni haramu kwa mwanamke mwenye hedhi kuketi msikitini na haya ni makubaliano ya madhehebu manne, ama kupita msikitini bila ya kuketi kama amejiamini kuwa hawezi kuchafua msikiti ataruhusiwa kama kama walivyoeleza wanachuoni wa madhehebu ya Shafii na ya Ahmad .
Na miongoni mwa dalili ya huu uharamu huu katika Quran ni kauli yake Allah pale alipotaja hatua miongoni mwa hatua za kuharamishwa pombe:
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنْتُمْ سُكَارَى حَتَّى تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّى تَغْتَسِلُوا
Enyi mlioamini !msikaribie swala,hali ya kuwa mmelewa,mpaka myajue yale mnayoyasema,wala hali ya kuwa mna janaba isipokuwa (mkiwa) ni wenye kuvuka (msikiti) mpaka mkoge .
النساء: ٤٣
Aya hii ni dalili ya uharamu wa mwenye janaba kuingia msikitini isipokuwa akiwa anakatiza na kupita bila ya kukaa ,na pia mwenye hedhi ni haramu kwake kama mwenye janaba kwa sababu wote wana sifa ya kuwa na hadathi kubwa .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa:Dhul-Qa’adah 3, 1442H ≈ Jun 13, 2021M.
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•