Anauliza je uzushi wa kusherehekea mazazi ya Mtume ni shari yake ni mbaya zaidi ya kula riba ,kuzini,wizi,kuuwa na kudhulumu ?
Jawabu:
Maneno hayo si sahihi kuyazungumza hivyo kwa ujumla,kwa sababu wanawachuoni walichosema ni kuwa kila bidaa ni upotevu na ijulikane kuwa bidaa ni uovu katika maovu na maovu yanatofautiana uzito wake,na imamu Asshatwibiy- Allah amrahamu – ameeleza kuwa bidaa imegawanyika makundi mawili kuna bidaa ambazo hukumu yake ni karaha na kuna zile ambazo hukumu yake ni haramu ,na pia akataja daraja za bidaa akasema :
Katika bidaa kuna zile ambazo ni ukafiri uliokuwa wazi , na kuna zile ambazo ni uovu tu hazifikii daraja la ukafiri, na kuna zile ambazo wanawachuoni wametofautiana ndani yake je ni ukafiri au si ukafiri kama vile bidaa ya (mapote yaliyopotea) kama Makhawarij ,na Al-Qadariyyah, na Murjia na mfano wa hayo katika mapote yaliyopotea ..
الأعتصام ٢٨٦/١
Baada ya utangulizi huo mfupi utajua kuwa kila bidaa ni upotevu na kumekuja makemeo makali ya moto kwa wazushi ,na uzushi mdogo huwenda ukamvuta mtu katika uzushi mkubwa na hii ni hukumu ya ujumla bila ya kuchanganuliwa na hapa utajua kuwa bila shaka zile bidaa kubwa kubwa kama vile : Uzushi wa (Rafidhwah) Ushia ,Ja’amiyyah,na mfano wa bidaa hizo mzito bila shaka bidaa hizi ni uovu zaidi kuliko madhambi mbalimbali kama vile kunywa pombe n.k ,lakini pia ifahamike kuwa madhambi makubwa kama vile Uzinifu ,wizi,kula riba n.k madhambi haya ni uovu zaidi kuliko bidaa nyingi za kimatendo kama vile kusherehekea mazazi ya Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- au kuleta dhikri kwa pamoja na mfano wa bidaa hizi na bila shaka ni katika upungufu wa kufikiri mtu akadhania kuwa mfano wa bidaa hizi kuwa ni uovu zaidi mbele ya Allah zaidi ya kunywa pombe,uzinifu n,k ,kwa hiyo maneno hayo aliyoyazungumza huyo mzungumzaji si sahihi kuyazungumza kwa sura hiyo labda kama angesema hivi:
“Bidaa ya kiitikadi ni uovu zaidi kuliko kula riba,kuzini,wizi,kuuwa na kudhulumu n,k”
Tanbih:
Tunawahusia walimu na wahatibu wanapozungumza maneno basi wayafafanue na kuyaweka wazi kwa sababu kitendo cha kuzungumza maneno kwa ujumla bila ya kuyafafanua huwenda mtu mwingine akakudhania vibaya kwa kutafsiri tafsiri usiyoikusudia ,kama alivyosema ibn l-Qayyim -Allah amrahamu-katika hili pale aliposema:
وعـلـيك بالتفصيل والتبيين فا
لإجمال والإطلاق دون بيان
قد أفسدا هذا الوجود وخبـطا
الأذهان والآراء كل زمـان
Nakamilisha maneno yangu kwa kunukuu maneno ya sheikh Swaleh Alu- sheikh -Allah amuhifadhi- katika sherehe yake ya kitabu “Fadhlu l-islam- pale aliposema -:
فجنس البدعة أشنع، وأغلظ من الكبائر ـ من جنس الكبائر ـ
Basi bidaa kama bidaa ni mbaya zaidi na (kosa lake ni) zito zaidi kuliko madhambi makubwa (kuliko) jinsi ya madhambi makubwa
لا يعني أن كل بدعة أعظم من كل كبيرة، لا، ولكن جنس البدع؛
Haina maana kuwa kila bidaa ni mzito zaidi kuliko kila dhambi kubwa hapana lakini bidaa kama bidaa (ina hukumu hiyo)
لأنها معارضة للرسول صلى الله عليه وسلم، واستدراك عليه،
Kwa sababu hiyo (bidaa inamaana ya) kumpinga Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-na kumrekebisha
وشرع دين لم يأذن به، وتعبد بأشياء لم تكن عليها سنته من جهة الاعتقاد، والشبهة،
Na kuweka dini asiyoruhusiwa (na Allah) na kuvifanya ibada vitu (ambavyo) havikuwa mwenendo wake (Mtume na anaweza kuyafanya haya ) kwa upande wa itikadi na shubha
وهذه أعظم من حيث الجنس من ذنوب الشهوات المختلفة.
Na haya (tuliyoyataja) ni makubwa zaidi kuliko (upande) wa jinsi ya madhambi mbalimbali ya matamanio.
المصدر : شرح فضل الإسلام
Hapo utaona kuwa tunatakiwa tuchunge maneno yetu pindi tunapozungumza hukumu za kisheria kwa kujilazimisha na yale maelezo waliyoyaeleza wanawachuoni.
Muandishi : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 16, 1445H ≈ Sep /19, 2024M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•