JE WANAWAKE WALIOOLEWA WANALIFAHAMU HILI?

ثبت في حديث أبي هريرة قال:

Imethibiti katika hadithi ya Abuu Hurairah – Allah amridhie – amesema:

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم

Amesema Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah zimfikie:

« إذا صلت المرأة خمسها وصامت شهرها وحصنت فرجها وأطاعت بعلها دخلت من أي أبواب الجنة شاءت »

“ Pindi mwanamke ataposwali swala zake tano, na akafunga mwezi wake (wa ramadhani), na akahifadhi tupu yake, na akamtii mumewe, ataingia katika mlango wowote wa pepo anaoutaka ”

📚 رواه ابن حبان.

و ثبت أيضا في حديث عبد الرحمن بن عوف قال:

Na imethibiti pia katika hadithi ya ‘Abdil-Rrahman bin ‘Auf amesema:

قال رسول الله صلى الله عليه وسلم –

Amesema Mtume wa Allah – swala na salamu za Allah zimfikie –

« إذا صلت المرأة خمسها وصامت شهرها وحفظت فرجها وأطاعت زوجها قيل لها ادخلي الجنة من أي أبواب الجنة شئت »

“ Pindi mwanamke ataposwali swala zake tano, na akafunga mwezi wake (wa ramadhani) na akahifadhi utupu wake na akamtii mumewe ataambiwa: Ingia peponi mlango wowote wa pepo unaoutaka ”

📚 رواه أحمد.

Maelezo kutoka kwa Mfasiri – Allah amuhifadhi

Mwanamke akiswali swala zake tano kwa kutimiza nguzo zake na sharti zake, na akafunga funga ya ramadhani yote kwa maana na yale madeni akayalipa na akauhifadhi utupu wake kutokana na machafu kama uzinifu na akawa mtiifu kwa mumewe katika mambo yasiyo kuwa ya haramu na katika huko kumtii mumewe ni pale atakapomuita kitandani kwa ajili ya kustarehe ni lazima aende sawa sawa mchana au usiku asikatae na wala asichukie bali anatakiwa aitikie wito wa mume kwa mapenzi na kwa kujipamba, labda ikiwa mke ni mgonjwa au yupo katika hali ambayo haruhusiwi kufanya tendo hilo, au labda mume akawa mlevi kisha akamuita mkewe hapo mke ana haki ya kukataa. Mwanamke akiyafanya mambo haya matano basi ataambiwa aingie peponi kwa kupitia mlango wowote autakao.

Tanbihi muhimu juu ya miongoni mwa sababu za mwanamke kupata ladha ya imani:

Unajua kuwa kwanini wanawake wengi hawapati ladha na utamu wa imani?

قال – صلى الله عليه وسلم

Amesema (Mtume) – Swala na salamau za Allah zimfikie

{ ولا تجد المرأة حلاوة الإيمان حتى تؤدي حق زوجها }

{ Na hatopata mwanamke ladha (tamu) ya imani mpaka atekeleze haki za mumewe }

📚 صحيح الترغيب (١٩٣٩)

Faida: ladha ya imani na furaha ya imani ni hali anayoihisi muumini, na mwanamke wa kiislamu hawezi akaipata ladha hii na utamu huu wa imani ambao haufanani na chochote katika dunia utamu ambao ni zaidi ya asali na sukari, utamu ambao mtu huhisi kana kwamba hayupo duniani, utamu ambao huona shida na mabalaa yote ya duniani si chochote na si lolote mbele ya pepo, na utamu huu mwanamke ataupata pindi atakapotekeleza haki za mumewe kama ilivyokuja katika hadithi tuliotaja hapo juu.

Tunamuomba Allah atupe furaha na mapenzi katika ndoa zetu.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Toleo la pili : Mfungo nane 7, 1443H ≈ Dec 11, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *