JE WAWAJUA WATU WABORA ZAIDI NA WATU WABAYA ZAIDI ?!

قال ابن القيم -رحمه الله-:

سمعتُ شيخ الإسلام يقول:

Amesema ibn l-Qayyim -Allah amrahamu – : Nimemsikia sheikh l-islam akisema :

كما أنّ خير الناس الأنبياء،
فشرّ الناس من تشبّه بهم من الكذّابين،
وادّعى أنه منهم، وليس منهم.

Kama (inavyofahamika) kuwa watu waliokuwa bora zaidi ni Manabii ,na watu wabaya zaidi ni wale waliojifananisha na hao (Manabii) katika waongo,na wakadai kuwa wao ni katika hao (Manabii) na (hali) si katika hao.

• فخير الناس بعدهم العلماء والشهداء والمتصدقون المخلصون،

Basi watu waliokuwa bora zaidi baada ya hao (Manabii) ni wanavyuoni, na Mashahidi, na wenye kutoa sadaka kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah.

فشرّ الناس من تشبّه بهم،
يُوهم أنه منهم، وليس منهم.

(ikiwa hivyo) basi watu wabaya zaidi ni wale waliojifanisha na hao, wakawafanya (watu) wawadhanie kuwa ni katika hao na (hali) si katika hao.

📚الداء_والدواء (ص٧٣).

Maelezo ya mfasiri :

Watu bora zaidi ni Mitume na Manabii kisha wanaofuata baada ya hao ni warithi wao nao ni wanavyuoni kama alivyoeleza Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie -:

” و إنَّ العلماءَ ورثةُ الأنبياءِ …“

Na hakika wanavyuoni ni warithi wa Mitume.

صحيح أبي داود .

kisha baada ya hao wanaofuata ni Mashahidi kwa maana wale waliouawa katika jihadi,kisha baada ya hao wanaofuata ni wale wanaotoa sadaka zao kwa ajili ya kutafuta radhi za Allah, na wala hawatoi kwa kutafuta sifa au kujionesha.

Kisha sheikh -Allah amrahamu -akasema kuwa :

Watu wabaya zaidi ni wale wanaojifananisha na hao waliotajwa hapo na hali wao si katika watu hao mfano :

1- Wanaojifananisha na Mitume kwa kudai kuwa wao ni Mitume kama vile Musailamatul -kaddhaab na wengineo wengi na bila shaka hawa ni watu waovu mno na waongo wakubwa na makafiri wakubwa!

2- Vilevile kuna wale wanaojifananisha na wanavyuoni kwa kudai kuwa wao ni wanavyuoni, na hawa pia ni watu waovu mno kwa sababu watu hawa humkosea Allah makosa makubwa ya kuzungumza katika dini yake bila ya elimu.

3- Vilevile kuna wale wanaojifananisha na wapiganaji jihad na hali si wapiganaji jihadi wa kweli ima kwa kutofuata sharti za jihadi au kwa sababu ya makusudio yao mabaya ya kutafuta sifa na cheo n. k.

4- Kundi la mwisho ni wale wanaojifananisha na wale wanaotoa kwa ajili ya Allah lakini wao hawatoi mali zao kwa ajili ya Allah bali hutoa kwa ajili ya makusudio mengine kama kujionesha au kutafuta sifa.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo pili 3, 1443H ≈ Jun 2, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *